Saturday, August 25, 2012

Barack Obama Ana Kiwanda Cha Bia ndani ya White House......



Kuongoza nchi kubwa kama Marekani yataka moyo! Ndio maana Barack Obama aliamua kuwa na kiwanda cha bia kwenye ikulu ya White House ili kupunguza stress za cheo hicho kikubwa duniani. Isitoshe kipindi hiki ni kigumu kwake kwakuwa anaelekea kwenye uchaguzi, so kupiga mtungi si jambo la kushangaza kwake.



 Amekuwa rais wa kwanza wa hivi karibuni nchini Marekani kunywa bia inayotengezwa kwenye Ikulu.
Bia inayotengenezwa humo imepewa jina la ‘White House Honey Ale’ ikiwa na rangi mbalimbali.

 Asali kidogo inayopatikana kwenye bia hiyo inatoka kwenye mizinga ya nyuki anayofuga mkewe Michelle Obama kwenye bustani yao.............

No comments:

Post a Comment