Wednesday, May 23, 2012

LISA JENSEN, OMMY DIMPOZ ‘IN LOVE’

Na Musa Mateja
KATIKA kuonesha kuwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya hasa masharobaro wamehamishia mapenzi yao kwa warembo, taarifa zilizotufikia zinadai Ommy Dimpoz yuko ‘in love’ na Miss Tanzania namba tatu 2006-07, Lisa Jensen.
Chanzo chetu cha kuaminika ambacho ni rafiki wa Ommy kimedai kuwa, wawili hao wana muda tangu wazame kwenye dimbwi la mahaba ila imekuwa ni kwa siri kubwa.
“Nyie si mnajua kufuatilia sana mambo ya watu? Sasa mbona mmeishia kuandika tu kwamba Diamond anatoka na Jokate halafu hamuandiki uhusiano wa Lisa na Ommy Dimpoz? Kama hamuamini fuatilieni mtaujua ukweli,” alisema mtoa habari huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Kujua ukweli wa ishu hii, mwandishi wetu alimtafuta Lisa ambaye alisema: “Duh! Kama demu wa Dimpoz ndiye anayenihusisha na madai hayo basi atakuwa na extra jealous (wivu wa kupitiliza), Dimpoz ni kaka tu.”
Kwa upande wa Dimpoz alifunguka: ”Lisa ni mshikaji wangu sana ndiyo maana napenda hata kuweka picha zake BBM, kama kuna lingine litajulikana tu.”
Souce:

No comments:

Post a Comment