Saturday, August 25, 2012

Barack Obama Ana Kiwanda Cha Bia ndani ya White House......



Kuongoza nchi kubwa kama Marekani yataka moyo! Ndio maana Barack Obama aliamua kuwa na kiwanda cha bia kwenye ikulu ya White House ili kupunguza stress za cheo hicho kikubwa duniani. Isitoshe kipindi hiki ni kigumu kwake kwakuwa anaelekea kwenye uchaguzi, so kupiga mtungi si jambo la kushangaza kwake.



 Amekuwa rais wa kwanza wa hivi karibuni nchini Marekani kunywa bia inayotengezwa kwenye Ikulu.
Bia inayotengenezwa humo imepewa jina la ‘White House Honey Ale’ ikiwa na rangi mbalimbali.

 Asali kidogo inayopatikana kwenye bia hiyo inatoka kwenye mizinga ya nyuki anayofuga mkewe Michelle Obama kwenye bustani yao.............

Facebook will disappear in the future....

Arcording to the expert's prediction, Facebook will be disappeared in next 5 to8 years . This information make the users in the internet tumult and worry in the recent weeks. However, the experts are not really shocked if it will happen reality.

Eric Jackson, founder of Ironfire Capital, said that in 5 to 8 years, Facebook will be disappeared in a way similar to Yahoo disappear. " Whether Yahoo is still making money, still profitable, still has 13 thousand employees working for them but they were only 10% in profit compared with their highest profit in 2000. That means unsuccessful and disappear
Jackson noted that, until this moment, the world has developed three generations of Internet companies. The first is Yahoo, a Web portal. This is a great example as a pioneer in the online field.Facebook then as the second generation with the wave of social media. The third generation is the world's mobile phone.

One of the problems for Facebook as the company can not make money from growing base of mobile phones. According to Jackson, Facebook will face challenges when moving into the mobile phone market like Google faced difficulties entering the field of social networks.

On the other side, predicted a collapse on Facebook comes just weeks after social networks have trouble with the IPO shares. Many financial analysts said that the company introduce the shares in the market was too high and it can never turn back to the first price.

Dan Olds, an analyst at consulting Gabriel Consulting Group agree with the views of Jackson, mobile phones will serve as increasingly important for any Internet company would, especially social networks . However, he believes too early to say Facebook will be thrown away of the mobile phone market.

Dan Olds said "Facebook is progressing slowly in the field of mobile phones. Most users see Facebook interface for mobile phone hardly to see. However, Facebook recently redesigned interface for mobile phones to view images more easily. But Facebook also needs to build a mobile business model so we can improve to attract advertisers.

Brad Shimmin, an analyst at CurrentAnalysis, agree with the view that, mobile phone is important, the foundation can help Facebook prosper and Facebook can also shield fall

Moshi Ufundi: Sekondari iliyogeuka kuwa magofu....(MOSH TECH)

HAINA CHOO, BAFU, WANAFUNZI WAJISAIDIA VICHAKANI.....


Kijana akipiga mswaki eneo la shule ya Sekondari ya Ufundi Moshi iliyopo Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro.













 SHULE ya Sekondari ya Ufundi Moshi iliyopo Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro ni miongoni mwa shule za Serikali iliyokuwa ikifanya vizuri kwa kutoa wasomi wengi miongoni wapo serikalini na taasisi binafsi.

Ilianzishwa mwaka 1957 ikiwa kama shule ya masomo ya biashara na ilipofikia mwaka 1967 ilibadilishwa na kuwa shule ya sekondari ya ufundi kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.

Kwenye miaka ya 1970 na 1980, ilikuwa na mazingira nadhifu kwa kuwa na majengo ya mabweni na vyumba vizuri vya kusomea. hali hiyo pia ilikuwa ikiandamana na matokeo mazuri kwa wanafunzi wengi.

Leo hii ukichunguza mazingira yake yalivyo ukalinganisha na hali na hadhi iliyokuwa nayo miaka 30 iliyopita waweza kupata wazo ambalo linawiana na msemo wa Kiswahili usemao: "Ngoma ikivuma sana mwisho wake hupasuka."

Sasa iko katika hali mbaya kiasi kwamba hata wanafunzi hawawezi kuingia msalani kutokana na miundombinu ya shule hiyo kuwa mibovu kupita kiasi.

Leo hii wanafunzi waalazimika kutumia choo kilichojenga mwaka juzi kwa ajili ya walemavu chenye matundu matatu ambacho kinatumiwa na wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha sita.

Mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo anasema vyoo na bafu vilijengwa tangu shule ilipoanzishwa na vimekuwa havifanyiwi ukarabati wala kujengwa vipya jambo ambalo limesababisha kuchakaa kiasi kwamba havifai kutumika.

Ukiingia baadhi utaona kuta zimoka sakavu imeharibika na vingi vinatiririsha maji machafu pembeni nu kusababisha vigeuke kuwa mazalia ya nzi, mende na wadudu wengine wanaotambaa.

Anasema wanafunzi wanashindwa kuvitumia vyoo hivyo mchana na mara nyingine wanajikuta wakilazimika kwenda kijisaidia kwenye vichaka karibu na shule hiyo.

Kutokuwa na maeneo ya kujisetiri faraga wakati wa kuoga, kumekuwa kukiwafanya wasubiri usiku wa giza ambao siyo rahisi kuonekana wao kwa wao au wapitanjia.

Alisema kufuatia uchakavu wa majengo, baadhi ya mabati yaliyoezekea majengo hayo yametoboka na wakati wa mvua yanavuja na hata kusababisha dari kuchakaa na mara kadhaa vipande vyake vimekuwa vikiwadondokea.

“Yaani hii shule iko katika hali mbaya kiasi kwamba hata sisi tunaosoma hapa tunaona tuko kama tunasomeshwa bure kumbe tunalipa ada na wazazi wanajua tuko katika shule nzuri. Kumbe mazingira haya ni mabaya," anasema mawafunzi huyo.

Uchakavu wa shule hiyo ipo hadi kwenye miundo mbinu ya usambazaji wa umeme na sasa majengo mengi hayana umeme jambo linalowalazimisha wanafunzi kutumia mishumaa wakati wa kusoma.

Licha ya uchakavu huo, wanafunzi wanalalamika kwamba wanafunzi wanaosajiliwa kila mwaka ni wengi kuliko uwezo wake.

“Kwa kweli! Kiwango cha elimu hapa shuleni kinashuka kutokana na mfumo wa shule ulivyo waalimu hawajali ni sawa na kwamba hawathamini kazi zao na mazingira wanayofanyia," anasema mmoja.

Anatoa mfano wa darasa lake kuwa lina wanafunsi zaidi ya 100 wakati uwezo wake halisi ni kati ya 45 hadi 50.

Anasema wakati mwalimu anafundisha, baadhi ya wanafunzi hushindwa kuingia darasani na kubakia kusikiliza wakiwa nje jambo ambalo linapunguza usikivu wa umakini.

“Wanafunzi wengi hawaingii darasani kwa kuwa unakuta hakuna sehemu ya kukaa wakiingia wengine wanakuwa wanazunguka tu na wala walimu hawasemi chochote,” analalamika mwanafunzi huyo.

Tatizo jingine ni shule hiyo kutokuwa na vifaa vya kufundishia wanafunzi walemavu, jambo ambalo linawapa shida kuendana na mazingira halisi ya ufundishaji hivyo kushindwa kupata elimu iliyokusudiwa.

Wanafunzi hao walisema walemavu walioko shuleni hapo hawatendewi haki kwa kuwa wanachanganywa na wanafunzi wakawaida bila kujali ni mlemavu wa aina gani.

“Hapa shuleni tuna walemavu ambao hawana uwezo wa kusikia sauti na wengine wasioona na vipofu na huwa tunachanganywa nao madarasani hawana waalimu wa kuwafundisha na unakuta hata hawaelewi chochote.” alisema.

Alisema baadhi ya waalimu hawaingii kufundisha darasani na pale wakijisikia na pale tunapohoji wanafunzi wanafukuzwa shule kwa kuwa hivi karibuni kuna baadhi ya viranja pamoja na wanafunzi ambao walihoji kuhusu ufundishaji na wote walifukuzwa.

Alisema wanafunzi wengi wamekuwa wanahofia kuzungumza hadharani matatizo ya shule hiyo kwa hofu ya kufukuzwa shule.

“Pamoja na ubovu wa vyoo, madarasa na mabafu hatuthubutu kulalamika kwa kuwa hofu ni kupatiwa barua ya kufukuzwa shule,” alilalamika.

Anadai kuna wanafunzi waliwahi kufukuzwa shule kutokana na kitendo cha kuhoji ratibu ya vyakula kwa sababu wanafunzi wamekuwa wakipikiwa Ugaki na maharage kila siku.

Anasema wanahofia maisha yao wakati wakiwa wamelala kutokana na bweni la wasichana kubomoka na wote kuhamia gorofa ya kwanza ambapo wanalazimika kulaa wanafunzi wanane hadi 10 katika chumba kimoja ambacho kina uwezo wa kulaza wanafunzi wanne.

Anaema gorofa ya juu ya jengo wanalolala limebomoka na hata ngazi zimevunjika kiasi kwamba ni hatari katika maisha yao.


“Tumelalamika kwenye uongozi wa mara kadhaa bila mafanikio,: lialaliachochote na ndio shule tuliopangiwa tukifikiria wengine wazazi wetu hawana uwezo wa kutuhamisha kwenda shle nyingine inatubidi tuvumilie shida hizi,” anasema.

Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo Maddy Kisuu, alikiri shule hiyo kukabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za uchakavu wa majengo, miundo mbinu na kushuka kiwango cha taaluma.

Kisuu anasema hali hiyo imechangiwa na Serikali kuongeza idadi ya wanafunzi wanaojiunga na shule hiyo huko miundombinu ya majengo ikiwa ni ile ile.

Anasema shule hiyo yenye wanafunzi 1,476 ina waalimu 17 na kusababisha kiwango cha elimu kushuka kupita kiasi kutokana na upungufu wa walimu.

Mkuu huyo anasema shule hiyo pia ina wanafunzi wenye matatizo ya kusikia 100 lakini ina walimu 5 kwa ajili yao jambo ambalo halitoshelezi kukidhi matakwa yao kikamilifu.

Anasema shule hiyo ni miongoni mwa zile zilizokuwa zikitoa wataalamu mbalimbali wa ufundi nchini lakini kwa sasa kiwango cha elimu kimeshuka kutokana na kukoza mazoezi kwa vitendo.

Katika kuthitisha hilo, anasema rekodi ya matokeo ya mithani wa kidato cha nne mwake 2007 yanaonyesha wanafunzi waliofaulu kwa daraja la kwanza 60 kati wanafunzi 230. Katika mwaka 2009 wanafunzi 14 tu kati ya 117 ndio waliofauli daraja la kwanza na na mwaka 2011 wanafunzi 29 kati ya 153 ndio walofaulu kwa daraja la kwanza.

Kwa matokeo ya kidato cha sita 2006 /2007 wanafunzi saba kati ya 152 ndio walifaulu kwa daraja la kwanza na 2007 /2008 hakukua na aliyefaulu kwa daraja la kwanza kati ya wanafunzi 101 na mwaka 2010/2011
waliofaulu kwa daraja la kwanza walikuwa tisa kati ya 151 na 2011/2012 wanafunzi wawili kati ya 183 ndio walifaulu kwa daraja la kwanza.

Kwa upande wa walemavu, hakuna aliyeweza kufaulu kwa miaka mitatu mfululizo iliyopita.

Wednesday, August 8, 2012

WATOTO WA MITAANI WATISHIA USAFI MOSHI MJINI.....

HALMASHAURIA ya Manispaa ya Moshi inakabiliwa na ongezeko la watoto wa mitaani wanaotishia kuibuka kwa vitendo vya uhalifu, huku mashirika ya Serikali na yasio ya Serikali yakitakiwa kusaidia kutoa elimu na ajira. Akizungumza mwishoni mwa wiki iliyopita, Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi, Bernadette Kinaboalisema halmashauri ina hofu baada ya ongezekola watoto wa mitaani,hali inayoweza kusababisha kuongezeka kwa vitendo vya ujambazi na magonjwa ya maambukizi. Kinabo alisema mwaka 2009 Manispaa ya Moshi ilikuwa na watoto wa mitaani 4,600, ambao walitoka familia za ndoa zilizovunjika ikiwamo umaskini uliowaondoa majumbani kwa kukosa huduma muhimu. Alisema zaidi ya nusu watoto hao wanasomeshwa na taasisi zisizo za Serikali na wengine wanasomeshwa kupitia magari (Mobile School ), badala yake wamekuwa wakirejea mitaani na kujitumbukiza katika vitendo viovu na uporaji. “Kwa kweli kila siku ziendavyo halmashauri inazidi kukabiliwa na ongezeko la watoto wa mitaani licha ya mji wetu kuwa msafi, wamekuwa wachafuzi wakubwa kwa baadhi ya maeneo,” alisema Kinabo. Kuhusu usafi wa mji huo, Kinabo alisema tangu mwaka 2006 ilipoweka sheria ndogo ya usafi wa mazingira ikisaidiana na sheria ndogo ya ada na ushuru ya mwaka huohuo, wamekuwa na mafanikio makubwa wa kuuweka mji wa Moshi katika hali ya usafi wa hali ya juu. Alisema mji huo umekuwa wa kwanza kwa usafi katika halmashauri 17 nchini kwa miaka mitano mfululizo, hivyo kuwafanya wageni wakiwamo watalii kutembelea mara kwa mara ikiwamo maeneo ya vivutio. Alisema hali hiyo imesababisha kutoa ajira kwa vikundi vya jamii na kupata ufadhili kutoka mji wa Delray Beach, nchini Marekani na kwamba, karibu watawasili hivi karibuni kuimarisha vikundi kazi kupitia mradi wao wa Manispaa ya Moshi.

Saturday, August 4, 2012

Zitto atoa ya moyoni kuhusu madai ya rushwa........

WAKATI shinikizo la kuvunjwa kwa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma (POAC), kwa tuhuma za ufisadi likiendelea, Mwenyekiti wake, Zitto Kabwe ameibuka na kukituhumu chama tawala CCM, Serikali na baadhi ya wapinzani akidai kuwa wana uchu wa kuiongoza kamati hiyo na wanaratibu mkakati wa kumchafua.

Kwa sababu hiyo, amepinga maoni ya baadhi ya wabunge wanaotaka ivunjwe na badala yake akasema kama kuna ushahidi wa kutosha dhidi ya vitendo vya rushwa, basi awajibike yeye.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Zitto alisema licha ya mkakati huo, katu hatarudi nyuma katika kutetea masilahi ya taifa kwa kuwa anaamini siku zote uongo hujitenga na ukweli.
“Mchango wa POAC katika Bunge na ustawi wa mashirika ya umma ni bayana na haujawahi kutiliwa shaka. Kamati yetu imeokoa upotevu mkubwa wa mali na fedha za umma kutokana na umakini wake,” alisema Zitto na kuongeza:

“Tumefanya hivyo CHC, Kiwira na kwenye mashirika mengi. Kote huku uadilifu wa kamati hii haujawahi kuhojiwa. Zipo hoja pandikizi za kutaka POAC ivunjwe na haswa zikinilenga mimi binafsi. Nafahamu kiu ya wasioitakia mema nchi yetu kuiona POAC ikivunjwa au sura zikibadilishwa kwa kuwa kamati hii imekuwa mwiba kwa mikakati yao ya kifisadi.”

“Kwa maoni yangu, POAC isihusishwe na tuhuma hizi kwa vyovyote vile. Niko tayari nihukumiwe mimi (Zitto) na siyo kuhusisha wajumbe wengine ambao hawatajwi mahala popote katika tuhuma hizi mbaya sana katika historia ya Bunge letu.”

“Nitakuwa tayari kunusuru Kamati ya POAC na masilahi ya taifa letu kwa kujiuzulu uenyekiti, iwapo itathibitika pasipo shaka kuwa nimehongwa. Kamati ya POAC ni muhimu kuliko mimi.”

Awali, Zitto alisema amelazimika kuzungumzia suala hilo kuufahamisha umma kwamba tuhuma hizo zenye shinikizo la kisiasa zinaelekezwa kwake binafsi na si kamati kwa jumla wake.
“Taarifa hizo, kama kawaida ya uzushi mwingine wowote, zimesambazwa kimkakati na kwa kasi kubwa, kiasi cha kuukanganya umma,” alisema.

Alisema mkakati wa kumuunganisha na baadhi ya wabunge wanaotuhumiwa kupokea rushwa, unatekelezwa kwa njia mbalimbali, ikiwamo kauli za watendaji wa Serikali aliodai wamekuwa wakizieneza kutoa taswira kwamba baadhi hoja zake zinatokana na ushawishi wa rushwa.

Akifafanua tuhuma za ushiriki wake wa rushwa katika sekta ya Nishati na Madini, Zitto alisema baada ya Bodi ya Wakurugenzi ya Tanesco kumsimamisha Mkurugenzi Mkuu, William Mhando, POAC ilimwomba Spika aridhie kamati yake iwaite wajumbe wa bodi hiyo ya Tanesco, CAG na PPRA, kujiridhisha na tuhuma hizo.

“POAC ilimwomba Spika kuwaita wahusika kwa kuwa zilikuwapo tetesi kuwa kusimamishwa kazi kwa mkurugenzi huyo kabla ya Bajeti ya Nishati na Madini kulikuwa na lengo la kufunika ‘madudu’ makubwa zaidi, kwa kulichagiza Bunge na tukio hilo dogo, mkakati ambao naona umefanikiwa sana,” alisema na kuongeza:

“Isitoshe, kamati kujiridhisha na hatua za bodi ni sehemu ya msingi ya utekelezaji wa majukumu yake yaliyowekwa kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge pia Tanesco ni moja ya mashirika ambayo yanawajibika kwetu kwa hesabu zake na ufanisi wake kwa jumla. Tumefanya hivyo katika mashirika mengi na hili la Tanesco siyo tukio la kipekee.”

“Binafsi sijawahi kuwa na mawasiliano ya aina yeyote na uongozi wa Tanesco, kushawishiwa juu ya hatua ambazo POAC ndiyo imezichukua za kutaka kujiridhisha juu ya utaratibu waliotumia.”
“Ieleweke wazi kabisa kuwa hakuna wakati wowote, popote ambapo mimi au kamati yetu imekataa Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco kuchunguzwa kwa tuhuma zozote. Ambacho tumesisitiza wakati wote ni ufuatwaji wa taratibu, kanuni na sheria, hili nitalisimamia iwe masika au kiangazi.”

Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya Chadema alisema kutokana na imani hiyo, anaunga mkono suala la tuhuma za rushwa zinazotajwa zichunguzwe na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa kina.

“Nakiomba pia chama changu, Chadema na vyombo vya dola vichunguze tuhuma hizo na kujiridhisha na ninaahidi kushiriki kikamilifu, iwapo nitatakiwa katika uchunguzi wowote utakaofanywa na niko tayari kuwajibika iwapo nitakutwa na hatia yoyote,” alisema.

“Napenda kuwatoa hofu wananchi wa Jimbo la Kigoma Kaskazini walionituma kuja kuwawakilisha hapa bungeni na Watanzania wote kwa jumla kwamba, mimi Zitto Kabwe sina bei, sijawahi kuwa nayo na sitarajii kuwa nayo huko mbeleni.”

“Daima nasimamia kidete maadili ya uongozi bora katika maisha yangu yote ya siasa na ninaahidi, sitarudi nyuma katika mapambano dhidi ya rushwa katika nchi hii pamoja na mikakati ya aina hii ya kunidhoofisha na kunivunja moyo.”

Zitto alilaani kile alichosema kuwa tabia iliyoanza kujengeka katika siku za hivi karibuni ya kuwamaliza wanasiasa wenye kudai uwajibikaji na uzalendo na kuanzishwa kiwanda kwenye medani ya siasa cha kuzalisha majungu na fitina, zenye lengo la kuwachonganisha wanasiasa wa aina hiyo na wananchi kwa kutumia nguvu za fedha.

Awashukia Profesa Muhongo, Maswi
Aliongeza kwamba, akiwa Dodoma amewahi kupata taarifa kwamba Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wake, Eliachim Maswi ndiyo wanaosambaza taarifa kwamba amepewa rushwa na Tanesco.

“Hali hii inaniondolea shaka juu ya ushiriki wao katika kueneza au kuthibitisha uvumi huo. “Ninajaribu sana kuzuia kutokuwa na shaka na ushiriki wao huo ikizingatiwa uzito na taswira ya nafasi zao katika jamii, lakini wameshindwa kunidhihirishia tofauti,” alisema.

Mbali na kuwatuhumu watendaji hao wa Serikali kwa kumchafua, Zitto alieleza kushangazwa na kauli zao kwamba mgawo wa umeme sasa basi, akieleza kuwa si kweli.

“Ili kumaliza tatizo la mgawo wa umeme kama alivyosema waziri na katibu mkuu, tunapaswa kuwa na Sh42 bilioni kila mwezi kuzilipa kampuni za IPTL na Symbion kama ‘service charge’, fedha hiyo haijatengwa kwenye Bajeti. Sasa msishangae baada ya wiki mbili mgawo ukarejea na watu watasema hizo ni njama za mafisadi,” alisema.

Zitto alisema waziri pia hakuwa sahihi kueleza kuwa Tanesco inapoteza Sh40 bilioni zinazotokana na mapato yake kwa mwezi baada ya matumizi ya Sh11 bilioni kwa kuwa hadi sasa shirika hilo la umma lina madeni mengi.

“Hivi inawezekana kweli maelezo hayo ya waziri kwamba kila mwezi Tanesco inatumia Sh11 bilioni kulipa mishahara na kupoteza Sh40 bilioni, zinazotokana na mapato yake? CAG yuko wapi na Kamati hii (POAC) iko wapi? Yaani wote sisi tusiyaone hayo ila yeye?,” alihoji.

Akizungumzia madai hayo ya Zitto, Profesa Sospeter Muhongo alisema: “Kila wakati tumekuwa tukizungumza juu ya jambo hilo, lakini hata hivyo, kama mnaweza kuangalia kupima uzito uko pande gani basi andikeni upande huo kati ya mimi na Zitto.”

Alisisitiza kwamba hakuna mgawo wa umeme na hilo ndilo analotaka Watanzania wafahamu na waondoe shaka na kamwe wasitegemee kusikiliza mawazo kutoka kwa watu ambao wanaamini kwa kufanya hivyo watajenga umaarufu.

Maswi hakupatikana jana kuzungumzia tuhuma hizo za Zitto baada ya simu yake ya mkononi kuita muda mwingi bila kupokewa na hata alipoandikiwa ujumbe mfupi hakujibu.

Spika aunda kamati maalum kuchunguza ufisadi bungeni...

KAMATI YA MAADILI YAWEKWA KANDO,KUKAMILISHA KAZI KWA WIKI MBILI...

SAKATA la tuhuma za ufisadi bungeni limeingia katika hatua mpya, baada ya Spika wa Bunge, Anne Makinda kuamua kuunda Kamati ndogo ya watu watano kuchunguza tuhuma za baadhi ya wabunge kuhongwa, kwa lengo la kushawishi uamuzi unaofaa kuchukulia katika chombo hicho cha kutunga sheria.

Uamuzi huo ambao Spika aliutangaza jana baada ya kipindi cha maswali na majibu Bungeni, unauweka kando ule wa awali, ambao ulikuwa ni kulipeleka suala hilo katika Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, ambapo alikuwa ameahidi kuwaengua wote watakaoonekana kuwa, wana mgongano wa kimaslahi na suala linalotakiwa kuchunguzwa.

Habari ambazo gazeti hili lilizipata zinadai kuwa, hadi jana wakati Makinda akichukua uamuzi huo, Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ilikuwa imeishaanza kazi kwa kufanya vikao kadhaa vya kuainisha watu ambao walipaswa kuitwa ili kutoa ushahidi na wengine kwa ajili ya kujibu tuhuma dhidi yao.

Makinda alisema Kamati hiyo itakayoongozwa na Mbunge wa Mlalo, Brigedia Jenerali Hassan Ngwilizi, itachunguza ukweli wa tuhuma hizo na kutoa majibu kwake ndani ya siku 14 kuanzia jana.

Alisema ameamua kufanya mabadiliko ya namna ya kushughulikia tuhuma hizo ili kutenda haki kutokana na unyeti wa suala hilo.

"Kwa kuzingatia misingi ya haki asili, tumeamua kutomweka mjumbe yeyote wa Kamati ya Nishati na Madini katika kamati hiyo," alisema Spika Makinda na kuongeza;

"Wajumbe wa kamati hiyo ni Mheshimiwa John Chiligati (Manyoni Magharibi), Riziki Omar Juma (Viti maalum), Said Amour Arfi (Mpanda Mjini) na Gosbert Blandes (Karagwe)."

Hata hivyo wajumbe wanne kati ya watano wanatoka ndani ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, isipokuwa Chiligati ambaye anaungana na wenzake akitokea katika Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.

Spika alibainisha kuwa, kamati hiyo imepewa majukumu ya kuchunguza tuhuma hizo na kujiridhisha kuhusu ukweli wake, kisha kumshauri (Spika) hatua za kuchukua.

Hatua hiyo ya Spika imekuja siku chache baada ya baadhi ya vyama vya siasa na wabunge, kuhoji usafi wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge hata ikapewa jukumu la kuchunguza tuhuma hizo.

Baadhi ya vyama vilivyoitilia shaka kamati hiyo ni NCCR Mageuzi, ambacho Mwenyekiti wake, James Mbatia alitaka Kamati hiyo pia ivunjwe na kuchunguzwa kwa tuhuma za ufisadi.

Chama kingine ni Chadema, ambapo mwanachama na Mnadhimu Mkuu wa kambi ya upinzani, Tundu Lissu alitaka zivunjwe kamati kadhaa badala ya kamati ya Nishati na Madini pekee.

Pia Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari aliomba mwongozo wa Spika akitaka Kamati za Bunge za Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) na ile ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), zivunjwe kwani tayari zilishatuhumiwa kwa rushwa.

Hadidu rejea
Spika Makinda alisema kuwa, moja ya majukumu ya msingi ya kamati ya kina Ngwilizi ni kukutana na kukubaliana namna ya kuendesha uchunguzi huo kwa haki na weledi.

"Kamati hiyo itatakiwa kupitia kumbukumbu ya taarifa rasmi za Bunge (Hansard) ili kujua michango ya wabunge wakati wa bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, kuwaita na kuwahoji mashahidi," alisema Spika Makinda.

Spika Makinda alimtaja Tundu Lissu kuwa ni shahidi muhimu katika uchunguzi huo, kutokana na hatua yake ya kuwataja baadhi ya watuhumiwa katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Dodoma.

Aliwataja mashahidi wengine katika uchunguzi huo kuwa ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, wabunge wote waliochangia Hotuba ya Wizara ya Nishati na Madini na kutoa tuhuma za rushwa na mbunge yeyote mwenye ushahidi.

"Tundu Lissu ni shahidi kwa sababu aliwahi kuwataja wabunge hao kwenye mkutano wake na waandishi wa habari na waziri ndiye aliyeanzisha tuhuma hizo bungeni," Spika Makinda alisema.

Aliongeza kuwa, kutokana na unyeti wa suala hilo, kamati hiyo inapaswa kuzingatia Katiba, Sheria, Kanuni za Bunge na weledi wa hali ya juu.

"Sasa waliotaka kuwataja wabunge hao humo bungeni sasa waende wakawataje kwenye kamati hiyo, alisema Spika Makinda," alisema.

Hata hivyo, jana mchana wakati wa kuahirishwa kikao cha Bunge cha mchana mbunge wa Muhambwe (NCCR-Mageuzi), Felix Mkosamali alihoji sababu za kamati hiyo kujaa wabunge watatu wa CCM huku chama chake kikiwa hakina hata mjumbe mmoja.

Lakini, hoja hiyo ilifafanua na mwenyekiti Jenister Mhagama aliyekuwa akiendesha Bunge kwani alisema isingekuwa rahisi kamati hiyo kujaza watu wengi.

Wanasayansi waazimia kuuangamiza Ukimwi,,,,,,,,,,,,,,

MBINU MPYA ZA KITAALAMU SASA KUTUMIKA DUNIA NZIMA  ......................

MKUTANO wa Ukimwi uliokuwa unafanyika Washington DC, Marekani umemalizika kwa wajumbe zaidi ya 2,000 kuridhia maendeleo ya kisayansi yaliyofikiwa kwa sasa wakisema ni madhubuti hivyo kutoa azimio la kuungana kuangamiza janga la maradhi hayo duniani. Moja ya maazimio yao ni kuifikisha dunia mahali ambako hakutakuwa na mtu atakayekufa wala atakayekuwa anaishi na Virusi Vya Ukimwi (VVU). Hii inatokana na matumaini ya kisayansi waliyohakikishiwa na watafiti juu ya kuwepo kwa dawa zinazoweza kuzuia maambukizo mapya na ambazo zikitumika kikamilifu zaweza kufanya kazi kama tiba.

Pamoja na kuwepo kwa dawa hizo, wamekiri kuwa mkakati huo hauwezi kufikiwa iwapo dunia haitajenga mshikamano wa pamoja wa kisera, uelimishaji na fedha za kutosha kufanikisha mbinu hizo mpya za kisayansi. Wanasayansi wametahadharisha kuwa kuwepo kwa dawa hiyo siyo tija ya kuumaliza Ukimwi kama mikakati imara haitawekwa dunia nzima. Rais wa Taasisi ya Kijamii ya Kimataifa ya Mapambano dhidi ya VVU (IAS), Dk Elly Katabira alisema yapo mambo mengi ambayo yalithibitishwa kisayansi huko nyuma lakini kwa kuwa hakukuwa na mikakati madhubuti, tatizo hilo limeendelea kuwa janga la dunia.

Dk Katabira ambaye pia ni mmoja wa watafiti wa kisayansi katika Chuo Kikuu cha Tiba cha Makerere, Uganda alitoa mfano wa watoto kuendelea kuambukizwa Ukimwi wanapozaliwa wakati tayari dawa ya kuondoa tatizo hilo ipo. “Ni jambo la kusikitisha kwamba dawa ya kuzuia maambukizo ya VVU tumekuwa nayo tangu miaka 1990 lakini mwaka huu, 2012 takwimu zinaonyesha kuwa watoto zaidi ya 300,000 wataambukizwa VVU wakati wa kuzaliwa,” alisema Dk Katabira, ambaye pia alikuwa ni Mwenyekiti wa mkutano huo wa Ukimwi uliomalizika wiki iliyopita.

Kwa sababu hiyo, akasema silaha za kupambana na Ukimwi kwa sasa zipo lakini kama hakuna mikakati madhubuti ya kuzitumia, bado utaendelea kuwa janga la dunia. Mkutano huo wa kimataifa wa Ukimwi umekuwa ukifanyika kila mwaka ukiwakutanisha wanasayansi na watunga sera kama vile wanasiasa na wadau wa mapambano dhidi ya ugonjwa huo uliogundulika kwa mara ya kwanza mwaka 1981.

Mkutano wa safari hii umeelezewa kuwa ni wa kipekee zaidi ukilinganishwa na ile iliyowahi kufanyika miaka 30 iliyopita kwani kwa mara ya kwanza, umethubutu kutamka wazi, “dawa ya kuangamiza kabisa janga la Ukimwi ipo.” Kutokana na kujiamini huko, mkutano huo umetoka na Azimio linaloitwa la Washington DC ambalo ni la kugeuza kauli ya kuwa “Ukimwi hauna dawa” na kuwa “Ni wakati wa kuangamiza janga la Ukimwi.”

Azimio hilo ambalo tayari limetafsiriwa katika lugha mbalimbali duniani, kikiwemo Kiswahili, linasema: “Kugeuza mkono kwa pamoja: Ilani ya kuangamiza janga la Ukimwi.” Linaeleza: “Tuko katika wakati wa kipekee katika historia ya janga la Ukimwi. Miongo mitatu ya upiganiaji, utafiti na utoaji wa huduma stahimilivu kwa jamii imeifikisha dunia katika hali ambayo haikuwazika miaka iliyopita.” “Kwa sasa kuna uwezekano wa kuanza kuangamiza janga la Ukimwi wakati wetu.

Hasara imekuwa ya kutohesabika… Lakini sasa, kupitia maendeleo mapya ya kisayansi… Tumegundua kwamba inawezekana kukusanya mbinu zilizothibitishwa, ambazo, kama zitatekelezwa ipasavyo, zinaweza kugeuza mkondo wa Ukimwi.” Ingawa tafiti za kisayansi zinaendelea na baadhi zikiwa na matumaini mazuri ya kupata dawa ya chanjo na kuponya waathirika dhidi ya VVU, bado hazijathibitishwa na azimio la mkutano huo limeridhia mbinu zilizowasilishwa na wanasayansi za kuzuia maambukizo.

Imeelezwa kwamba mbinu hizo mpya za kuzuia kusambaa kwa VVU zikitumika kikamilifu siyo tu zitazuia maambukizo mapya, bali zitatibu wale waliokwishaambukizwa. Moja ya mikakati ya kufanikisha azimio hilo ni kuhakikisha duniani kote vinapatikana vifaa bora vya kuchunguza VVU na upatikanaji wa dawa. “Lazima tuongeze rasilimali na bidii yetu kwa kutumia vifaa tulivyonavyo leo kuzuia maambukizo mapya na kuboresha afya ya mamilioni ya watu walio na VVU/Ukimwi. Mamilioni ya maisha yataokolewa,” inaeleza sehemu ya Azimio hilo la Washington DC na kuongeza:

“Lengo la kwanza ni kuangamiza janga la Ukimwi... Liko katika uwezo wetu... Hakuna mtu anapaswa kutengwa ikiwa tunapanga kufikia lengo letu.” Miongoni mwa mambo ambayo azimio hilo linasisitiza kuwa hayana budi kuzingatiwa ili kuleta usawa ni pamoja na kuondoa unyanyapaa, ubaguzi, vikwazo vya kisheria na unyanyasaji wa haki za waathirika na wale walio hatarini. “Unyanyapaa na ubaguzi unazuia juhudi zetu zote na kuzuia utoaji wa huduma muhimu. Tuongeze kwa dhahiri upimwaji wa VVU, utoaji ushauri na uhusiano wa kinga, huduma za kuponya na usaidizi. Kila mtu ana haki ya kujua hali yake ya VVU na kupata matibabu, dawa na usaidizi,” linasisitiza azimio hilo.

Malengo mengine ni kutoa matibabu kwa wanawake wote wajawazito na wanaonyonyesha wanaoishi na VVU na kuangamiza uambukizaji wakati wa kujifungua. Azimio linahamasisha ujengaji wa mtandao mpana wa vita hiyo kwa kusema: “Tuongeze ufikio wa matibabu ya kupunguza makali ya VVU/Ukimwi kwa wote wanaohitaji.

Hatuwezi kuangamiza Ukimwi mpaka mikakati hii iweze kutekelezeka ulimwenguni kote.” Linaongeza: “ Tuharakishe utafiti kuhusu vifaa vipya vya kukinga na kutibu VVU, ikiwa ni pamoja na njia mpya kama vile tiba ya kuzuia maradhi kabla ya kuambukizwa (PrEP) na vizuizi vya vijiumbe maradhi na utoaji bora wa kile tunachojua kinafanya kazi ipasavyo; kuanzia kondomu mpaka matibabu kama kinga.

Tuongeze utafiti wa dawa ya chanjo na dawa ya kuponya. Utafiti ni muhimu kwa kutusaidia kupigana na janga hili.” Tayari Dawa ya Kupunguza Makali ya VVU (ARV) ya Truvada iliyonza kutumika duniani tangu 2004, wiki chache zilizopita ilithibitishwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa Marekani (FDA), kuwa ina uwezo wa kuzuia mtu aliyeathirika kumwambukiza mwenzi wake atakayeshiriki naye tendo la ndoa bila kutumia kondomu. Zipo aina kadhaa ya dawa za chanjo na tiba zilizowasilishwa kwenye mkutano huo pamoja na ushahidi wa jinsi zinavyoponya lakini bado hazijathibitishwa kutumika kimataifa.

Thursday, August 2, 2012

CREATIVITY.......!!!

THE WAY  TO GET GOOD IDEAS IS TO GET LOTS OF IDEAS AND THROW THE BAD ONES AWAY...says the son of maletho!!!
PEACE... Peace of mind attained not by ignoring problems but by solving them....

Diaspora Writer"Muimbaji Chameleon kutoka Uganda ni Mwizi sana Hapa Uingereza amesha tapeli watu kishenzi,,,,,

Muimbaji chameleon kutoka Uganda ni mwizi sana .Hapa Uingereza amesha tapeli watu kishenzi staili hio hio na maneja wake. Ni mchezo wake.Akirudi hapa UK anaweza kupigwa mawe.Bangi zina msumbua tuu.Yeye ninani mtu amabe hawezi kumuheshimu mwakilishi wa Rais wetu Uganda -Balozi wetu pale kampala.Nashanga serikali ya Uganda wamemsikiliza na kuifanya hii ishu itake kuharibu uhusiano mkubwa kati ya nchi hizi mbili.Hivyo chameleone mnamjua ? juzi kawa muislam kesho yake karutadi tena .Bangi haziwezi zina mpelekesha. Anafaa kua jela maana ni msani jambazi.Huko kampala na sikia wamesha rushiana risasi na msani Bobby wine. Naomba watanzania wote tumzomeye chameleon na asirudi tanzania tena kwa tabia yake tena . Hon membe tunaomba hili ulifanyie kazi kwamba wageni hawezi kuja na wakatu abuse hata nyumbani kwetu. Bwana Erik nawe usije uka shika pasport ya mtu ni document ya serikali wala sio mtu binafsi
Ahsante
Diaspora writer