Mwanamuziki na producer anayemiliki studio ya Sharobaro Records, Bob Junior aka Mr. Chocolate Flava, ameamua kufungua ndoa kwa style ya aina yake.
Amesema harusi yake itakayofanyika jumapili ya tarehe moja mwezi July mwaka huu, pamoja na kufanyika nyumbani itatinga ndani ya club ya Billicanas ambapo kila mtu anaruhusiwa kuhudhuria.
Rais huyo wa masharobaro amesema wiki hii atapanda boti hadi Zanzibar kwenda kumfuata ‘mwali’ ili aisaliti rasmi kambi maarufu ya makapela.
Bob Junior anayesifika kwa kukata ‘mauno’ kwenye video zake, amesema amechoka kuishi maisha ya ujana na sasa anahitaji kuwa na familia.
“Tunapiga show kila siku na kupata hela nyingi kwanini nisioe,” aliiambia 255 ya Clouds Fm jana.
Aliongeza kuwa dhumuni la kuamua kuoa ni kuepukana na vishawishi na maradhi kwakuwa watu maarufu kama yeye hujikuta wakitafutwa sana na wasichana.
Kila lakheri Bob Junior.
Saturday, June 30, 2012
Wednesday, June 27, 2012
BELL9 NA BEN POL WATOA NYIMBO MPYA...
Nyimbo inaitwa ANAYEISHI NAE...its good sana find it and listenig it soon iwill keep it on my blog...THEY SHINE MEN...SAFI BELL9 NA BEN...great job!!!!
Mwana FA atangaza Vita na Wezi.....
“Next time nikikuta watu wanapiga mwizi na mtu akanizuia nisishiriki ntaanza na yeye kwanza” ni tweet ya Hamisi Mwinjuma aka MwanaFA iliyokuwa imeambatanishwa na picha ya gari lake lenye namba T 809 PMB ikiwa imenyofolewa taa zote za mbele na nyuma.
Wizi huo umefanyika usiku wa tarehe 24june.. na inavyoekena ni kuwa wezi walipanda na kuvuka geti kimya kimya, kwa raha zao wakanyofoa taa na kuingia ndani kuchukua radio.
Ile MwanaFA kuamka asubuhi ndo akakuta tayari wajanja wameshamliza kiasi cha kuamua kutangaza vita na wezi. Hivyo kama ukikuta MwanaFA anashiriki kumponda ‘vitofa’ mwizi aliyekamatwa street baada ya kuiba, kamwe usishangae, usimuulize na usimzuie sababu ataanza na wewe! Pole sana Binamu!
Hata hivyo wezi hao hawaikuiharibu ratiba ya usiku wa kuamkia leo ya Binamu. Ratiba yake ilianzia pale the so-called ‘Uwanja wa taifa wa burudani’ Dar Live ambapo aliperform ngoma yake mpya Ameen kwa mara ya kwanza.
Baada ya Dar Live show ikahamia Maisha Club, “Dar Live Done..Beautiful..Maishani Sasa Kwa Ndege Mnana,” alitweet.
Huko New Maisha Club alienda kumpa support mwanadada Linah Sanga aliyekuwa akifanya show yake ya kwanza tangu arudi kutoka kwenye ziara ndefu ya nchini Marekani. “What a show..Maisha I Loooooooooved you tonite!” aliandika alfajiri hii.
Baada ya kupata mtoto,Mr. Blue aongeza speed kumalizia mjengo wake...
Wiki iliyopita msanii wa kizazi kipya, maarufu sana nchini Herry Sameer aka Mr.Blue alijaaliwa kupata mtoto wa kiume aliyezaa na mchumba wake Wahida Mohamed.
Kwakuwa huyo ndio mtoto wa kwanza, Kabayser aliamua kumpa jina lake mwenyewe yaani ‘Herry’.
Funny enough siku tumempigia siku kuconfirm habari za kupata mtoto na kumuuliza kajaaliwa mtoto wa jinsia gani, Blue alijibu, “Ni jembe mshikaji wangu!!” akimaanisha mtoto wa kiume.
So baada ya kuongeza jina jingine halali mjini la ‘Baba Herry’, Mr Blue amesema inabidi aongezee kasi ya kumalizia mjengo wake anaoujenga jijini Dar es Salaam ili yeye,Mama Herry na Herry wakae kwa raha zao pamoja.
Alivyoongea na East Africa Radio siku zilizopita, Kabayser amesema baada ya miaka miwili nyumba yake inaweza ikawa imekamilika.
Kwa sasa Wahida na Mr. Blue kila mmoja anaishi nyumbani kwao.
Katika hatua nyingine siku chache baada ya kupata mtoto msanii huyo alisema mtoto wake akikua hapendi afanye muziki kama yeye kwakuwa hapendi awe maarufu.
“Mimi ningependa mwenyezi Mungu amjalie awe mtu fulani ambaye kidogo atakuwa hata kiongozi kusaidia watu,” alisema.
UNAJUA ALIYE MTOA DIAMOND????nani yuko nyuma ya mafanikio yake!!check out!!!
DIAMOND NA RUGE AKIMPA MAELEKEZO!!!
Ulishajiuliza kwanini Diamond yuko smart sana kwa namna anavyozipeleka issue zake za muziki? Hushangai iweje msaniii huyu ambaye wengi walitegemea awe na elimu ya chuo kikuu ndio aweze kuufanya muziki kwa umaridadi mkubwa kiasi cha kutochuja kwa show zake japo zinajipanga kama mayai kwenye tray!
Well, wengi hili wanaweza kuwa wanalijua juu juu tu ama hawalijui kabisa kuwa the person behind Diamond’s music creativity is none other than Ruge Mutahaba!!
Yeah, habari ndio hiyo, hate it or love it.
Tangu show ya aina yake ya Diamonds Are Forever iliyowapa mkwanja mnene wa kuweka benki na kula bata, show ya Dar Live iliyompa sifa Diamond kwa kutua kwenye ‘Uwanja huo wa taifa wa burudani mpaka show ya Big Brother Stargame aliyoifanya mwaka huu. He (Ruge) was the mastermind!
Ameweza kumtengeneza Diamond kuwa bidhaa ya thamani isiyochuja.Hautakosea ukimwita Russell Simmons wa Tanzania. Kwa uzoefu alionao kupitia show zinazoandaliwa na kituo cha Clouds Fm, ameweza kuzijua ramani zote za kupitia ili kufanikiwa ‘kibiashara’ kwenye muziki wa Tanzania. He has the music map in the palm of his hands and never missed a shot!
Kuna mtu mmoja wa karibu sana na Diamond hivi karibuni ametuambia kuwa maandalizi ya show ya ‘Diamonds Are Forever ya pale Mlimani City yalichukua takribani wiki nzima. Ruge alikuwa akienda kila siku kuangalia maendeleo ya rehearsal and he was like, “mmh mmh! Hapo bado,ongezeni nguvu zaidi.”
Kwenye show ya hivi karibuni ya Miss Redds Tanzania huko Arusha, Ruge alionekana kwenye picha akimwelekeza Diamond namna ya kupiga kinanda na ngoma. Haijalishi kama anajua kupiga hivyo vitu ama la,hilo si suala letu, cha msingi ni kuwa ushauri wake unafanya kazi kwa Diamond.
And tell you what, hakuna mtu mwenye connection ya masuala ya muziki iwe ndani ya nchi ama nje kama Ruge! Hivyo kuchuja kwa Diamond katika ramani ya muziki wa kibiashara bado sana.
Ndani ya Mj-Recordz Diamond Akifanya Tangazo la Coca Cola...work hard man!!!GOOD!!!!...
Well, wengi hili wanaweza kuwa wanalijua juu juu tu ama hawalijui kabisa kuwa the person behind Diamond’s music creativity is none other than Ruge Mutahaba!!
Yeah, habari ndio hiyo, hate it or love it.
Tangu show ya aina yake ya Diamonds Are Forever iliyowapa mkwanja mnene wa kuweka benki na kula bata, show ya Dar Live iliyompa sifa Diamond kwa kutua kwenye ‘Uwanja huo wa taifa wa burudani mpaka show ya Big Brother Stargame aliyoifanya mwaka huu. He (Ruge) was the mastermind!
Ameweza kumtengeneza Diamond kuwa bidhaa ya thamani isiyochuja.Hautakosea ukimwita Russell Simmons wa Tanzania. Kwa uzoefu alionao kupitia show zinazoandaliwa na kituo cha Clouds Fm, ameweza kuzijua ramani zote za kupitia ili kufanikiwa ‘kibiashara’ kwenye muziki wa Tanzania. He has the music map in the palm of his hands and never missed a shot!
Kuna mtu mmoja wa karibu sana na Diamond hivi karibuni ametuambia kuwa maandalizi ya show ya ‘Diamonds Are Forever ya pale Mlimani City yalichukua takribani wiki nzima. Ruge alikuwa akienda kila siku kuangalia maendeleo ya rehearsal and he was like, “mmh mmh! Hapo bado,ongezeni nguvu zaidi.”
Kwenye show ya hivi karibuni ya Miss Redds Tanzania huko Arusha, Ruge alionekana kwenye picha akimwelekeza Diamond namna ya kupiga kinanda na ngoma. Haijalishi kama anajua kupiga hivyo vitu ama la,hilo si suala letu, cha msingi ni kuwa ushauri wake unafanya kazi kwa Diamond.
And tell you what, hakuna mtu mwenye connection ya masuala ya muziki iwe ndani ya nchi ama nje kama Ruge! Hivyo kuchuja kwa Diamond katika ramani ya muziki wa kibiashara bado sana.
Ndani ya Mj-Recordz Diamond Akifanya Tangazo la Coca Cola...work hard man!!!GOOD!!!!...
Tuesday, June 19, 2012
MBUNGE WA UBUNGO...John Mnyika atolewa nje mbugeni leo..
KATIKA BUNGE LA BAJETI 2012/2013 katika mkutano wa nane katika hoja za serikali....leo tarehe 19/6/2012 saa 12:00 mbunge wa ubungo john mnyika katika kuchangai maada alitoa kauli ya kusema "UDHAIFU WA RAIS KIKWETE", "UPUUZI NA UPUMBAVU WA WABUNGE/ NA WA CCM"katika kutoa hujo naibu spika aka muomba afute hyo kauli ila akasema hatoweza kufuta kwa kuwa anahoja ya kutete kuhusu hlo ila haikutosha waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu akismama na kusoma kifungu cha sheria ya bunge kuhusu maneno yaliyosemwa na john mnyika...ALL AT ALL mh mnyika akasimama na kusema kwel kauli yangu sitoi..ila naibu spika akasimama na kufuata sheria na kumtoa katika kikao cha bunge cha leo mpaka kesho saa tatu!!!
DAH....KWEL BUNGE LA SASA......NDIO BUNGE...TUPIA COMMENT IS IT RIGHT???
Monday, June 18, 2012
Bunge kuwaka moto wiki hii.......
MKUTANO wa nane wa Bunge la Jamhuri ya Muugano wa Tanzania unaingia katika wiki ya pili leo, huku kukiwa na kila dalili za kuwapo mjadala mkali wa hotuba ya bajeti iliyowasilishwa bungeni Alhamisi iliyopita na Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa.Miongoni mwa mambo yanayotarajiwa kuiweka njiapanda Serikali ni suala la deni la taifa ambalo kwa mujibu wa bajeti iliyosomwa limefikia karibu Sh 20.3 trilioni Machi mwaka huu, kwani wabunge wanataka mchanganuo wa jinsi deni hilo lilivyofikia kiwango hicho.
Suala jingine ambalo linaweza kuzua mvutano ni kile wabunge wanachodai kuwa ni ukaidi wa Serikali kutosikiliza mawazo yao miaka nenda rudi kwa kutotenga fedha za kutosha kwa ajili ya maendeleo.
Katika bajeti yake ya 2012/2013, fedha za maendeleo zilizotengwa na Serikali ni asilimia 30, lakini wabunge wanataka kiwango hicho kiongezwe hadi asilimia 35 na matumizi ya kawaida yabakie 65.
Kadhalika bajeti hiyo, Serikali itakuwa na wakati mgumu kutokana na wabunge wengi kunusa ufisadi katika bajeti ya 2011/2012 kutokana na fedha kidogo zilizopelekwa katika wizara na idara za Serikali, ilhali taarifa za mapato ya nchi zikionyesha kwamba fedha nyingi zilikusanywa na Mamlaka ya Mapato (TRA) hadi asilimia 106.
Suala la kutokuwapo kwa uwiano kati ya mapato na matumizi ya Serikali, ndilo liliwasukuma baadhi ya wabunge wa CCM waliohudhuria kamati ya wabunge wa chama hicho Ijumaa iliyopita, kuibua hoja ya kutaka kuchunguzwa kwa mfuko mkuu wa Serikali kwa maelezo kwamba kuna dalili za kuwapo kwa ufisadi.
Uchambuzi rasmi wa bajeti hiyo utaanza kufanywa na Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi kupitia maoni yake yanayotarajiwa kusomwa na Mwenyekiti wake, Andrew Chenge na kufuatiwa na Bajeti mbadala ya Kambi ya Upinzani, inayotarajiwa kuwasilishwa na Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi, Zitto Kabwe.
Chenge tayari alishasema kwamba, kamati yake imeelewana na Serikali kwa ahadi ya kurekebisha kasoro za kibajeti katika mwaka ujao wa fedha, lakini baadhi ya wabunge wa CCM katika kikao chao Ijumaa, waligeuka mbogo wakitaka marekebisho makubwa yafanywe.
Kadhalika baadhi ya wabunge hao wa CCM waliripotiwa kutohudhuria kikao hicho kukwepa kuwa sehemu ya makubaliano ambayo yangefikiwa na ‘kuwafunga midomo’ wakati wa kuchangia bajeti hiyo wiki hii.
Licha ya kutengwa fedha kidogo, pia wabunge kadhaa wa CCM na wale wa upinzani wanapinga matumizi makubwa ya Serikali na kupuuzwa kwa mpango wa Serikali wa kubana matumizi, hasa kupunguzwa safari za nje na za ndani za viongozi, kulipana posho, makongamano na mikutano.
Wakati wabunge wa CCM wakiendelea na mkutano wao Ijumaa, Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina alijitokeza mbele ya waandishi wa habari na kutangaza kwamba hataunga mkono bajeti hiyo na kwamba, yuko tayari kufukuzwa ndani ya CCM kutokana na hatua yake hiyo.
Hoja ya Mpina ni kutaka Serikali ifumue bajeti yake na aliahidi kwamba leo ataomba mwongozo wa Spika ili kutoa hoja ya kutaka bajeti isijadiliwe na badala yake Serikali ipate fursa ya kuifanyia marekebisho makubwa, ikiwa ni pamoja kuongezwa kwa fedha za miradi ya maendeleo kutoka asilimia 30 hadi 35 ya bajeti, pia kupunguzwa kwa matumizi yasiyo ya lazima.
Hoja hiyo ya kushauri bajeti kufumuliwa, pia ilijadiliwa katika kikao cha ndani cha wabunge wa CCM, ambapo Mbunge wa Mwibara, Alphaxard Lugola na Mbunge wa Kilindi, Beatrice Shelukindo, ambao waliungwa mkono na wabunge wengine kadhaa, walinukuliwa wakibainisha upungufu mkubwa uliopo ikiwa ni pamoja na fedha kidogo za miradi ya maendeleo.
Katika kikao hicho, pia wabunge hao, walieleza kutoridhishwa na utekelezwaji wa bajeti katika wizara nne, kutokana na kutengewa fedha kidogo, lakini miradi kutotekelezwa kwa wakati kama ambavyo ilikusudiwa.
Wizara ambazo zilitajwa ni pamoja na Nishati na Madini, Uchukuzi, Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika na Wizara ya maji.
“Katika Wizara ya Nishati na Madini kuna miradi ambayo ilipaswa kutekelezwa badala yake, wakati wa kipindi hiki cha mwisho cha maandalizi ya bajeti, zimekwenda kuwekwa nguzo tu, ili kuonyesha kuanza kwa miradi….Sasa jambo kama hili halifai,” Lugola alinukuliwa akisema ndani ya kikao hicho.
Kutokana na umuhimu wa mjadala wa bajeti, tayari wabunge kadhaa walishajiorodhesha kuchangia mjadala hata kabla ya bajeti kusomwa, lakini Naibu Spika, Job Ndugai alisema wiki jana kuwa kanuni za Bunge zinaruhusu wabunge kujiorodhesha kuchangia baada ya kusomwa bajeti.
Subscribe to:
Posts (Atom)





