Wednesday, June 27, 2012

UNAJUA ALIYE MTOA DIAMOND????nani yuko nyuma ya mafanikio yake!!check out!!!

DIAMOND NA RUGE AKIMPA MAELEKEZO!!! Ulishajiuliza kwanini Diamond yuko smart sana kwa namna anavyozipeleka issue zake za muziki? Hushangai iweje msaniii huyu ambaye wengi walitegemea awe na elimu ya chuo kikuu ndio aweze kuufanya muziki kwa umaridadi mkubwa kiasi cha kutochuja kwa show zake japo zinajipanga kama mayai kwenye tray!
Well, wengi hili wanaweza kuwa wanalijua juu juu tu ama hawalijui kabisa kuwa the person behind Diamond’s music creativity is none other than Ruge Mutahaba!!
Yeah, habari ndio hiyo, hate it or love it.
Tangu show ya aina yake ya Diamonds Are Forever iliyowapa mkwanja mnene wa kuweka benki na kula bata, show ya Dar Live iliyompa sifa Diamond kwa kutua kwenye ‘Uwanja huo wa taifa wa burudani mpaka show ya Big Brother Stargame aliyoifanya mwaka huu. He (Ruge) was the mastermind!
Ameweza kumtengeneza Diamond kuwa bidhaa ya thamani isiyochuja.Hautakosea ukimwita Russell Simmons wa Tanzania. Kwa uzoefu alionao kupitia show zinazoandaliwa na kituo cha Clouds Fm, ameweza kuzijua ramani zote za kupitia ili kufanikiwa ‘kibiashara’ kwenye muziki wa Tanzania. He has the music map in the palm of his hands and never missed a shot!
Kuna mtu mmoja wa karibu sana na Diamond hivi karibuni ametuambia kuwa maandalizi ya show ya ‘Diamonds Are Forever ya pale Mlimani City yalichukua takribani wiki nzima. Ruge alikuwa akienda kila siku kuangalia maendeleo ya rehearsal and he was like, “mmh mmh! Hapo bado,ongezeni nguvu zaidi.”
Kwenye show ya hivi karibuni ya Miss Redds Tanzania huko Arusha, Ruge alionekana kwenye picha akimwelekeza Diamond namna ya kupiga kinanda na ngoma. Haijalishi kama anajua kupiga hivyo vitu ama la,hilo si suala letu, cha msingi ni kuwa ushauri wake unafanya kazi kwa Diamond.
And tell you what, hakuna mtu mwenye connection ya masuala ya muziki iwe ndani ya nchi ama nje kama Ruge! Hivyo kuchuja kwa Diamond katika ramani ya muziki wa kibiashara bado sana.

Ndani ya Mj-Recordz Diamond Akifanya Tangazo la Coca Cola...work hard man!!!GOOD!!!!...

No comments:

Post a Comment