Wednesday, June 27, 2012
Baada ya kupata mtoto,Mr. Blue aongeza speed kumalizia mjengo wake...
Wiki iliyopita msanii wa kizazi kipya, maarufu sana nchini Herry Sameer aka Mr.Blue alijaaliwa kupata mtoto wa kiume aliyezaa na mchumba wake Wahida Mohamed.
Kwakuwa huyo ndio mtoto wa kwanza, Kabayser aliamua kumpa jina lake mwenyewe yaani ‘Herry’.
Funny enough siku tumempigia siku kuconfirm habari za kupata mtoto na kumuuliza kajaaliwa mtoto wa jinsia gani, Blue alijibu, “Ni jembe mshikaji wangu!!” akimaanisha mtoto wa kiume.
So baada ya kuongeza jina jingine halali mjini la ‘Baba Herry’, Mr Blue amesema inabidi aongezee kasi ya kumalizia mjengo wake anaoujenga jijini Dar es Salaam ili yeye,Mama Herry na Herry wakae kwa raha zao pamoja.
Alivyoongea na East Africa Radio siku zilizopita, Kabayser amesema baada ya miaka miwili nyumba yake inaweza ikawa imekamilika.
Kwa sasa Wahida na Mr. Blue kila mmoja anaishi nyumbani kwao.
Katika hatua nyingine siku chache baada ya kupata mtoto msanii huyo alisema mtoto wake akikua hapendi afanye muziki kama yeye kwakuwa hapendi awe maarufu.
“Mimi ningependa mwenyezi Mungu amjalie awe mtu fulani ambaye kidogo atakuwa hata kiongozi kusaidia watu,” alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment