Mwanamuziki na producer anayemiliki studio ya Sharobaro Records, Bob Junior aka Mr. Chocolate Flava, ameamua kufungua ndoa kwa style ya aina yake.
Amesema harusi yake itakayofanyika jumapili ya tarehe moja mwezi July mwaka huu, pamoja na kufanyika nyumbani itatinga ndani ya club ya Billicanas ambapo kila mtu anaruhusiwa kuhudhuria.
Rais huyo wa masharobaro amesema wiki hii atapanda boti hadi Zanzibar kwenda kumfuata ‘mwali’ ili aisaliti rasmi kambi maarufu ya makapela.
Bob Junior anayesifika kwa kukata ‘mauno’ kwenye video zake, amesema amechoka kuishi maisha ya ujana na sasa anahitaji kuwa na familia.
“Tunapiga show kila siku na kupata hela nyingi kwanini nisioe,” aliiambia 255 ya Clouds Fm jana.
Aliongeza kuwa dhumuni la kuamua kuoa ni kuepukana na vishawishi na maradhi kwakuwa watu maarufu kama yeye hujikuta wakitafutwa sana na wasichana.
Kila lakheri Bob Junior.
No comments:
Post a Comment