RAIS Jakaya Kikwete ameteua wakurugenzi wapya tisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambao pia watakuwa na hadhi ya Balozi, akiwemo Msaidizi wa Rais (Hotuba), Mbelwa Kairuki. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mjini Dar es Salaam leo na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, uteuzi huo umeanza Mei 2, mwaka huu. Walioteuliwa ni Vincent Kibwana anayekuwa Mkurugenzi, Idara ya Afrika; Naimi Aziz (Idara ya Ushirikiano wa Kikanda); Celestine Mushy (Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa); Yahya Simba (Idara ya Mashariki ya Kati), na Bertha Somi (Idara ya Diaspora). Wengine ni Irene Kasyanju (Kitengo cha Sheria); Dorah Msechu (Idara ya Ulaya na Amerika); Kairuki ( Idara ya Asia na Australia), Silima Haji (Idara ya Mambo ya Nje, Zanzibar). Kabla ya uteuzi wake, Kibwana alikuwa Ofisa Mambo ya Nje Mkuu, Aziz alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Mushy alikuwa Kaimu Katibu wa Waziri Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Simba alikuwa Ofisa Mambo ya Nje Mkuu, na Somi alikuwa Ofisa Mambo ya Nje Mkuu. Naye Kasyanju alikuwa Mkurugenzi Msaidizi; Msechu alikuwa Mkurugenzi Msaidizi na Kairuki alikuwa Msaidizi wa Rais (Hotuba), Ofisi ya Rais, Ikulu na Haji alikuwa Ofisa Mambo ya Nje Mkuu.
Thursday, May 31, 2012
Rais Kikwete ateua wakurugenzi wapya Mambo ya Nje....

Wanafunzi Chuo Kikuu wabakwa, walawitiwa...!!!!!
WANACHUO wa Chuo Kikuu cha St John mjini Dodoma, leo wamegoma kuingia madarasani hadi wawasilishe malalamiko yao kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Zelothe Stephen kutokana na kukithiri kwa vitendo vya kupigwa nondo, kuibiwa kadi za benki, kompyuta za mkononi, kulawitiwa na kubakwa.
Hali hiyo ilisababisha wanafunzi kukusanyika huku wakiwa wamebeba mabango mbalimbali ambayo yalikuwa yakisomeka, ‘Tunaomba ulinzi ili kubaka na kulawitiwa kukomeshwe’, ‘Ulinzi ni haki yetu ya msingi polisi Mko wapi? Tumechoka kuwa wajinga katika jamii yetu na Ulinzi Shirikishi stop crime.’
Baadhi ya wanafunzi hao walilaani vitendo vya wenzao kubakwa na kulawitiwa na kudai kuwa katika siku za hivi karibuni, mwanafunzi wa kiume ambaye anasoma mwaka mwaka wa pili aliibiwa na kisha kulawitiwa hali iliyolazimu alazwe hospitali.
“Kesi kadhaa zimepelekwa polisi lakini hakuna chochote kinachofanyika,” alisikika mwanachuo moja akizungumza kwa jazba.
Walisema kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na wakati mgumu kutokana na kuibiwa vifaa muhimu zikiwemo kompyuta za mkononi hali ambayo hulazimika kuishi kwa hofu.
“Juzi wenzetu wamevamiwa usiku na kuporwa simu tano na laptop tatu sasa tunaona maisha yanakuwa magumu sana kwetu kwani usalama wetu sasa ni mdogo,” alisema mmoja wa wanafunzi hao.
Walisema hali ni mbaya zaidi kwa wanafunzi ambao wanaishi nje ya chuo kwani hata kujisomea nyakati za jioni kumekuwa kwa mashaka kutokana na kuogopa kuvamiwa na vibaka.
Walisema baadhi ya wenzao wanaanza mitihani Juni, hali ambayo inawatia hofu kama wimbi hilo la kuvamiwa na vibaka linaweza hata kupunguza ufaulu mioungoni mwao.
Pia walitaja sababu kadhaa ambazo zinadhaniwa kuwa zinasababisha matukio hayo ni chuo hicho kukosa uzio na hivyo kufanya mwingiliano wa watu na wanachuo kuingia chuoni bila kuwa na utaratibu.
Walisema kundi lisilojulikana limekuwa na kawaida ya kuvamia sehemu ambazo wanachuo wanakaa na baada ya kuiba vitu mbalimbali humalizia kwa kubaka wasichana au kwa kulawiti kama ni mvulana.
Hata hivyo, juhudi za wanafunzi wao kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma hazikufanikiwa baada ya kuelezwa kuwa alikuwa na majukumu mengine ya kikazi, na kutuma mwakilishi wake ambaye ni Mkuu wa Polisi Wilaya, Dominic Mlei na Mkuu Mpya wa Polisi wa Wilaya atakayeanza kazi hivi karibuni, Thadeus Malingumu.
Kwa upande wake, OCD Mlei alisema ulinzi unaanza rasmi leo, kufanya doria maeneo yanayozunguka chuo hicho na maeneo jirani, pia chuo kijenge hosteli za kutosha na kwa kila hosteli za nje na nyumba walizopanga wanafunzi zitakaguliwa kesho na mapungufu ya kiusalama kwenye makazi hayo yataainishwa na wamiliki wataitwa na hosteli zote zitatakiwa kuwa na mageti na ulinzi wa makazi hayo kuboreshwa.
Pia alitaka kuundwa kwa mara moja kwa vikundi vya ulinzi shirikishi.
Hata hivyo, mtumishi wa Chuo hicho, Mzee Muganda alishauri Kituo Kidogo cha Polisi kijengwe Kikuyu na bidii ya doria iongezwe.SASA WAMEAMIA DODOMA...SIKU SIO CHACHE HABARI HIZI ZILIKUWA SANA KATIKA CHUO CHA SAUT MWANZA....ILA SERIKALI INAPASWA KULITILIA MAKZO SWALA HILI.......
Wednesday, May 30, 2012
Sugu (Mbunge) Kutoa Kutoa Barudani Dar Live Jumapili Hii
Mwanamuziki mkongwe wa Hip Hop nchini Joseph Mbilinyi aka ‘M II’ au ‘Sugu’ amethibitisha kuwa siku ya Jumapili ijayo (Juni 3) atatoa shoo ya nguvu ndani ya Ukumbi wa Taifa wa Burudani wa Dar Live huko Mbagala, jijini Dar es Salaam
Mhasibu Lindi kortini kwa kumjeruhi mkewe kwa pasi...
MKAZI wa Kata ya Wailes katika Manispaa ya Lindi Bw. Mwanzaga Mbowi amefikishwa Mahakama ya Mkoa wa Lindi akikabiliwa na shitaka la kumjeruhi mkewe kwa kumchoma na moto wa pasi.
Bw. Mboi ambaye ni Mhasibu katika Manispaa hiyo alipandishwa kizimbani Mei 28, mwaka huu na kusomewa shitaka lake na Mwanasheria wa Serikali, Bi. Mwahija Ahamadi.
Akisomewa shitaka lake mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo Bw. Dustan Ndunguru, Mwanasheria wa Serikali alidai kuwa mshitakiwa alitendo kosa hilo Mei 27, mwaka huu, saa 1:30 asubuhi.
Bi. Mwahija alidai kuwa siku hiyo ya tukio huko Wailes iliyopo katika Manispaa ya Lindi mshitakiwa alimjeruhi mke wake wa ndoa Bi. Olifoncia Chembekwa kwa kumchoma na moto wa pasi.
Aliiambia mahakama hiyo kwamba siku na wakati huo mshitakiwa na mke wake kwa pamoja walikuwepo nyumbani kwao na mara kukatokea kidogo mifarakano ambayo ilipelekea mshitakiwa kumpiga na hatimaye kuchukua pasi ya moto na kumuunguza mlalamikaji mkono wake wa kulia na sehemu nyingine.
Mwendesha mashitaka huyo alidai kutokana na kitendo hicho, mshitakiwa alimsababishia mlalamikaji maumivu makali kwenye mwili wake.
Bi. Mwahija aliiambia Mahakama hiyo kwamba kutokana na kitendo hicho mshitakiwa amefanya kosa chini ya kifungu cha 225 Kanuni ya Adhabu Sura ya 16.
Hata hivyo Mshitakiwa alikana kosa linalomkabili na kupelekwa rumande baada ya upande wa mashitaka kupinga dhamana kwa mshitakiwa kutokana na kutopata taarifa ya maendeleo ya mlalamikaji huku kesi hiyo namba 49/2012,itatajwa tena Juni 11, mwaka huu.

Kagasheni asimamisha vigogo wanne Tanapa...
Ni kuhusiana na mauaji ya faru
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, ameanza kazi kwa kishindo katika wizara hiyo baada ya kuwasimamisha kazi maofisa wanne wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) na Serengeti na askari 28 kutokana na uzembe uliosababisha kuuawa kwa faru wawili katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Kagasheki ambaye kabla ya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri alikuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam, alisema maofisa hao wamesimamishwa kazi kuanzia juzi yaani Mei 28 mwaka huu ili kupisha uchunguzi dhidi yao tukio hilo utakaofanywa na tume itakayoundwa.
Aliwataja maofisa hao kuwa ni Kaimu Mkurugenzi wa Uhifadhi Tanapa, Justin Hando, Mkuu wa Kitengo cha Intelejensia Tanapa, Emilly Kisamo, Mkuu wa Hifadhi ya Serengeti, Mtango Mtahiko na Mratibu wa Miradi ya Faru Serengeti, Mafuru Nyamakumbati.
Kagasheki aliwataja pia askari 28 wanaolinda doria katika hifadhi ya Serengeti ambao nao wamesimamishwa kuwa ni Askari Mwandamizi Fatael Mtu, Rashid Athuman, Mohamed Athuman, John Fabian, Goodchance Msela, Joseph Darus, Emmanuel Ishalila na Felician Gwangu ambao wote ni askari wa daraja la pili.
Alisema askari wa daraja la tatu waliosimamishwa ni Jafari Hassan, Malale Mwita na John Urio wakati wa daraja la nne ni Majuto Omari, Deogratias Waisiku, Chacha Ndege, Samson Njoghomi, Leonard Kunjumu, Siad Mkamba, Paul Cosmas, Gabriel Ngazama.
Wengine ni Rajab Mangachi, Adam Likarawe, Anodisu Mushumali, John Zimbi, Drigue Shaabani, Rashid Mangandali, Edson Mbyazi, John Mbilizi na Emmanuel Kilawe.
Alisema maofisa na askari hao wamesimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi utakaofanywa na tume atakayoiunda kwani wameonyesha uzembe mkubwa kutokana na kutotoa taarifa za kuuawa kwa faru hao wizarani tangu tukio hilo lililopotokea Aprili mwaka huu na badala yake serikali ikapata taarifa hizo kupitia vyombo vya habari.
“Faru wameuawa tangu mwezi Aprili mwaka huu, lakini Tanapa walisema tukio hilo walilijua, lakini hawakutoa taarifa kwa wizara kitu ambacho kinatia shaka kwamba huenda kuna baadhi yao walihusika kwa namna moja au nyingine katika tukio hili,” alisema Kagasheki.
Alisema Tanapa ndiyo wasimamizi wa hifadhi za taifa na kwamba kutotoa taarifa kwa wizara ni tatizo na udhaifu mkubwa wa kiutendaji na kuonya kuwa hataweza kuvumilia kuona vitendo vya aina hiyo vinaendelea katika wizara hiyo.
Kagasheki alisema katika Wizara hiyo jamii imejenga dhana kwamba ni sehemu ambako kuna uchafu mwingi na wanaofanya vitendo hicho hawachukuliwi hatua jambo ambalo alidai chini ya uongozi wake atahakikisha anafuta dhana hiyo kwa wahusika kuchukuliwa hatua mara moja.
“Kumetokea mabadiliko ya mawaziri na sababu ni nyingi, katika wizara hii ya Maliasili na Utalii kuna sura ya wizara imejengeka kwamba kuna uchafu mwingi, wengine wanasema hii ni wizara ya mali za siri wakimaanisha kwamba vitendo vichafu vinafanyika katika wizara, lakini wahusika hawachukuliwi hatua,” alisema Kagasheki.
Alisema tukio la faru kuuawa lazima kuna siri iliyojificha ama kuna baadhi ya waliosimamishwa wamehusika kwa namna moja au nyingine kwani haiwezekani majangili waingie ndani ya hifadhi na kufanya tukio hilo huku watu waliopewa dhamana ya kulinda hifadhi wapo na wamelijua tukio hilo lakini wamenyamaza.
“Hii vita siyo ndogo ni kubwa lakini naahidi tutapambana, maana haiwezekani tukio limetokea mwezi Aprili mwaka huu halafu wahusika wamenyamaza kimya tu hawatoi taarifa, nahisi kuna uhusiano wa tukio hilo na baadhi ya watumishi waliosimamishwa,” alisema Kagasheki na kubainisha kuwa tume itakapomaliza kazi watakaobainika kuwa hawakuhusika hawatachukuliwa hatua.
Faru waliouawa Aprili mwaka huu ni jike mmoja aliyejulikana kwa jina la Sarah na mtoto wake ambapo mizoga yao ilikuwa katika eneo la Hifadhi ya Serengeti bila pembe.
Tukio la kuuawa kwa faru limekuwa la pili naada ya lile la mwaka jana faru mwingine aliyejulikana kwa jina la George (12) maarufu kama ‘Faru wa JK’ aliuawa na baada ya tukio hilo Serikali iliahidi kuimarisha ulinzi wa wanyama hao kwa kutumia vifaa maalum vya mawasiliano ili kufuatilia mienendo yao.
Kuuawa kwa faru mwingine mwezi uliopita kumewashtua baadhi ya wahifadhi wa Tanapa kiasi cha kufanya kuwa la siri kubwa huku watawala wakikwepa kutoa taarifa za suala hilo wizarani.
Kagasheki ameanza kuchukua hatua za kukabiliana na vitendo vya ufisadi katika wizara hiyo, zikiwa siku chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kumuondoa aliyekuwa waziri wa wizara hiyo, Ezekiel Maige, katika mabadiliko ya baraza la mawaziri yaliyofanywa Mei 4, mwaka huu.
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, ambayo iliwasilisha taarifa yake bungeni katika Mkutano wa Saba ikimtuhumu Maige kushindwa kudhibiti ubadhirifu katika wizara yake kama ulivyobainika katika ugawaji wa vitalu vya uwindaji wa kitalii na usafirishaji wa wanyama hai nje ya nchi.
Tuesday, May 29, 2012
Idd Simba kizimbani!!!!!!
NI KUJIBU MASHTAKA YA UFISADI UDA, AJIDHAMINI KWA MALI YA SH8 BILIONI BADALA YA SH500 MILIONI ILIYOTAKIWA......
Tausi Ally na James Magai MWENYEKITI wa Bodi ya Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda) Ltd, Iddi Simba, jana alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka manane, likiwemo la matumizi mabaya ya madaraka na kulisababishia shirika hilo hasara ya Sh2.4 bilioni.Mbali na Simba ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, washtakiwa wengine ni Meneja Mkuu wa Uda, Victor Milanzi na Mkurugenzi wake Salim Mwaking’inda ambaye pia aliwahi kuwa Diwani wa Kata ya Sinza (CCM).
Baada ya Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Benny Lincoln kumaliza kuwasomea mashtaka yanayowakabili, aliieleza mahakama hiyo kuwa upelelezi wa kesi hiyo umeshakamilika na wanaomba kesi ipangiwe tarehe ya kutajwa kabla ya kupangiwa tarehe ya maelezo ya awali. Wakili Said El- Maamry anayemtetea Simba na mwenzake, Alex Mgongolwa waliiomba Mahakama impatie dhamana mteja wao hoja ambayo haikuwa na pingamizi kutoka kwa Lincoln ambaye alisema mashtaka yanayowakabili washtakiwa yanadhaminika.
Ili kujidhamini, Hakimu Mfawidhi, Ilvin Mgeta aliwataka washtakiwa kutoa hati ya nyumba na kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika, kila mmoja wao asaini bondi ya Sh500 milioni.
Baada ya kutolewa kwa masharti hayo, Simba aliwasilisha hati ya nyumba yenye thamani ya Sh8 bilioni na kuridhia wenzake waitumie kupata dhamana.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa hati hiyo ya nyumba ni ya kiwanda cha Kays Hygiene Products Ltd, kilichoko Mikocheni eneo la Viwanda, Plot namba 23, kinachomilikiwa na Simba na mkewe Khadija.
Simba ni Mwenyekiti wa Taasisi ya mikopo kwa Wajasiriamali ya Pride (T) Ltd na Mwenyekiti wa Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam. Akisoma hati ya mashtaka jana Lincoln alidai kuwa Septemba 2, 2009 Dar es Salaam, Simba na Milanzi walikula njama ya kuchepusha fedha kinyume na Kifungu cha 29 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 11 ya 2007.
Lincoln alidai kuwa Simba na Milanzi walighushi barua wakionyesha kuwapo kwa kiwango zaidi cha fedha kwenye akaunti zote za benki za Uda wakati wakijua kuwa si kweli. Aliongeza kuwa siku hiyo hiyo, Simba na Milanzi kwa pamoja, walichepusha Sh320 milioni wakijifanya ni malipo ya awali ya mauzo ya hisa katika shirika hilo fedha ambazo walijipatia kutokana na nyadhifa zao.
Aidha, kati ya Septemba 3, 2009 na Machi 31, 2010, Simba na Milanzi wanadaiwa kujipatia Sh320 milioni kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa Robert Simon Kisena wakijifanya ni sehemu ya malipo ya hisa za Uda. Lincoln alidai kuwa washtakiwa Simba na Mwaking’inda kati ya Septemba 2009 na Februari 2011, wakati wakitekeleza majukumu yao, kwa makusudi walitumia vibaya nafasi zao waliharibu hisa milioni 7,880,330 zisizotumika za Uda ambalo ni shirika linalomilikiwa kati ya Serikali Kuu na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam zinazokadiriwa kuwa na thamani ya Sh1,142,643,935 bila kufuata taratibu za zabuni kitendo ambacho ni uvunjwaji wa masharti ya Kanuni ya 63 (1) ya Ununuzi ya umma.
Washtakiwa hao wote kwa pamoja wanadaiwa kuwa kati ya Septemba 9 na Februari 11, 2011 wakitekeleza majukumu yao, kwa makusudi walitumia vibaya madaraka yao kwa kugawanya hisa 7,880,330 zisizotumika za UDA kitendo ambacho ni uvunjwaji wa masharti ya vifungu vya ushirikiano katika kampuni na Kifungu cha 74 cha Sheria ya Makampuni Sura ya 212 iliyorekebishwa mwaka 2002.
Mwendesha mashtaka huyo wa Takukuru, alidai kuwa Februari 11, 2011 washtakiwa hao walishindwa kuchukua tahadhari zinazostahili, walimuuzia Simon hisa milioni 7,880,303 zisizotumika za Uda kwa bei ya Sh1,142,643,935 bila kufuata utaratibu wa zabuni ambao ungeweza kutoa nafasi kwa mnunuzi kutoa ofa ya bei inayolingana na thamani ya hisa hizo, jambo ambalo liliisababishia Uda hasara ya Sh2,378,858,878.80

Sunday, May 27, 2012
Diva wa Clouds FM kumshirikisha Diamond kwenye wimbo wake!
Bila shaka kupita Blog ya Kidbway Leotainment ulipata taarifa kuwa mtangazaji wa Clouds FM Loveness aka Diva anatarajia kujaribu bahati yake kwenye muziki wa Bongo Flava kuona upande huo wananchi watampokeaje.
Updates za story hii ni kuwa Diva huyo atamshirikisha pia Diamond kwenye wimbo utakaotengenezwa na Lamar.
Taarifa hizo zimethibitish
wa na Diamond mwenyewe kupitia twitter ambapo alikuwa akimjibu mtangazaji wa Radio Citizen na Citizen TV za Kenya, Willy Tuva "Kuna kibao nitafanya na Diva wa Clouds chini ya Fish crab cookout"
Diva ambaye hujiita ‘Mimi’ ni miongoni mwa watangazaji wanaozungumzwa zaidi nchini kwa mabaya mengi na mazuri machache kutokana na aina ya utangazaji wake kwenye kipindi cha Ala za roho katika kituo hicho cha radio maarufu kwa burudani nchini kutokana na sifa yake ya kuongea mambo mazito ya kimapenzi bila kificho.
Diva anategemea kuachia wimbo utakaojulikana kwa jina la ‘Piga Simu’ chini ya producer Lamar wa Fish Crub!
(May 24) Lamar ametweet “Diva aka mimi under xclusive muzik the lebal !soon to release a hit song piga simu.”
Yetu masikio kujua kama Diva atajikusanyia mashabiki pia katika muziki baada ya kufanya vizuri upande wa radio ama atawatukana tena wanaume!
Mtangazaji huyo amelazimika kuomba radhi baada ya kusema kwenye kipindi chake kuwa wanaume wa kitanzania ni wachafu,wananuka boxer,midomo,vikwapa n.k.
Unadhani Diva anaweza kuwa mwanamuziki mzuri?

DIAMOND ACHAFUA UKWENI....dah....plantinum nawe..
ILE skendo ya kunaswa hotelini na mcheza sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel bado inamtesa mwanamuziki Naseeb Abdul ‘Diamond’ ambapo safari hii anadaiwa kuchafuka vibaya upande wa wakwe zake kwa mchumba’ke Jokate Mwegelo, Ijumaa linafunguka.
Habari kutoka kwenye chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa wawili hao zinadai kuwa baada ya habari hiyo kubumburuliwa na gazeti damu moja na hili, Risasi Jumamosi ndiyo iliyotibua mambo ukweni kwake hivyo kuonekana siyo.
MSURURU WA WANAWAKE
Ilidaiwa kuwa habari hiyo ndiyo iliyotonesha kidonda kilichokuwa kinataka kukauka cha ‘kichaa’ huyo wa Bongo Fleva kutajwa kutoka kimapenzi na msururu wa wanawake mastaa na wasiokuwa mastaa.
“Asikwambie mtu, unajua upande wa akina Jokate ni watu wa dini sana. Yaani kwa skendo skendo kama hizo, wanamuona Diamond kama anataka kuwachafua.
“Unajua zile ishu za kudaiwa kutoka kimapenzi na msururu wa wanawake zilikuwa zimeanza kutulia kwa sababu yupo na Jokate lakini baada ya kutokea hii ya kunaswa hotelini na Aunt, imetibua mambo kule ukweni na mbaya zaidi anaonekana hajatulia,” kilisema chanzo hicho kwa sharti la kutochorwa jina gazetini.
HUYU HAPA DIAMOND
Ili kupata mzani wa habari hiyo, Ijumaa lilimvaa Diamond kavukavu ambapo katika kuthibitisha kuwa vyanzo vyetu vya habari havibahatishi, alikiri kuchafuka ukweni huku akiongeza kuwa anahisi kuna watu nyuma ya habari hizo ambao wamelenga kumharibia mambo yake.
“Naomba niweke wazi jambo hili kwa sababu ni kweli nachafuliwa.
“Kuna watu wananichafua ili nionekane kituko kwenye familia ya akina Jokate, nahisi wanaweza kufanikiwa,” alisema Diamond Platnumz.
UHUSIANO WAKE NA JOKATE
Kufuatia ishu hizo, uhusiano wa kimapenzi wa kidume huyo na mwanamitindo Jokate unadaiwa kuwa kwenye hatihati pamoja na kwamba bado wapo pamoja.
TULIKOTOKA
Mwishoni mwa wiki iliyopita Diamond na Aunt walidaiwa kubambwa katika Hoteli ya Kebby’s iliyopo Mwenge, Dar wakila ‘good time’, hivyo kuzua tafrani kwenye uchumba wa mwanamuzi huyo na Jokate.
Mbali na madai hayo yanayomhusisha Diamond na Aunt ‘kuminya’ pamoja, kichwa hicho cha Bongo Fleva kiliwahi pia kutajwa kutoka na mwigizaji Jacqueline Wolper, wauza nyago kwenye video za muziki, Rehema Fabian na Natasha, staa wa Maisha Plus, Pendo Moshi kabla ya kumchumbia Wema Sepetu kisha wakamwagana na kujikuta mikononi mwa Jokate.

Uwoya, Patcho(tajiri) Wapeleka Arobaini ya Kanumba Congo
Patcho Mwamba.
Na Shakoor Jongo
MASTAA wanaotamba katika filamu za Kibongo, Irene Pancras Uwoya na Patcho Mwamba ‘Tajiri’ Mei 23, mwaka huu wameupeleka msiba wa staa mwenzao, marehemu Steven Kanumba huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kwa ajili ya maombolezo.
Wakizungumza na Ijumaa muda mchache kabla ya kukwea pipa, mastaa hao walisema wamepewa mwaliko na baadhi ya wafanyabiashara wa nchini humo kwa ajili ya kwenda kumalizia msiba wa Kanumba.
“Unajua kifo cha Kanumba kimewagusa watu wengi, siyo Watanzania tu, hata kule kwetu pia kulikuwa na maombolezo, kwa kuwa arobaini imeshapita wametupa mwaliko kwenda kujumuika nao,” alisema Patcho ambaye pia ni mwanamuziki wa Bendi ya FM Academia.
Mei 17, mwaka huu, Kanumba alitimiza siku 40 tangu alipofariki na shughuli za kumalizia msiba zilifanyika jijini Dar kwa baadhi ya ndugu zake na mastaa kutembelea kaburi lake na kituo cha watoto yatima cha Kuwama

Mwakyembe akesha na abiria waliokwama Tazara....
WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe juzi usiku alikesha na abiria zaidi ya 1,000 waliokwama kwa saa 11 katika stesheni ya Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (Tazara) jijini Dar es Salaam kutokana treni kukosa mafuta.
Kutokana na tatizo hilo, Dk Mwakyembe ambaye alifika katika stesheni hiyo mara baada ya kuwasili kutoka safarini India, aliahidi kuwashughulikia watendaji wa Tazara waliosabab
isha uzembe huo.
Dk Mwakyembe ambaye ametimiza siku 20 tangu alipoteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuongoza Wizara ya Uchukuzi, alifika eneo hilo baada ya abiria wawili kumpigia simu na kuomba aingilie kati tatizo hilo.
Alifika stesheni katika hiyo saa 4:01 usiku na kukaa mpaka saa 6:30 usiku alipoondoka na hakukuwa na kiongozi yeyote wa ngazi za juu wa Tazara aliyefika kushughulikia tatizo hilo. Akutana na abiria Baada ya Dk Mwakyembe kuwasili na kuingia katika ukumbi wa kupumuzika abiria wanaposubiri kuondoa, wasafiri walimshangilia kwa nguvu mara baada ya kujitambulisha kuwa ni Waziri wa Uchukuzi na amefika kutatua tatizo linalowakabili, ingawa ni usiku akiwa ametoka safarini India.
Abiria hao waliokuwa na jazba walimwelezea waziri huyo kuwa kufika kwake eneo hilo ni uzalendo ambao hawakuutegemea na kutaka awapatie majibu ya chanzo cha tatizo na namna atakavyolitatua.
Awali, Kabla ya kuingia ndani ya ukumbi huo, uliibuka mvutano wa chini kwa chini baina yake na baadhi ya watendaji na wanausalama waliotaka asingie ukumbini kwa hofu ya kufanyiwa vurugu abiria hao waliokuwa na hasiri.
Lakini Dk Mwakyembe aliwataka watendaji wamfungulie mlango ili aingie ndani ya ukumbi kukutana na abiria hao.
Alipofunguliwa mlango, Dk Mwakyemba akiwa ameongozana na baadhi ya wafanyakazi wa mamlaka hiyo waliokuwa zamu, aliingia ndani ya ukumbi na umati wa watu walimzunguka huku kila mmoja akitaka kuwakilisha kilio chake.
Mmoja wa abiria hao alipasa sauti na akisema; “Tunataka uje huku, mpaka muda huu hatujaondoka, hatuelewi chochote, hatujui kama treni itaondoka au hapana, na kama itaondoka itakuwa saa ngapi? Hawa Tazara wanadharau, wanatutesa! Tunaomba uje utusikilize na ueleze kama safari ipo au la”. Dk Mwakyembe aliwatuliza akisema; “Tulieni, tulieni! Nimekuja hapa kwa sababu baadhi yenu wamenipigia simu kunieleza kuwa mmekwama hapa kwa muda mrefu na mnahiji msaada ili muweze kuondoka.
“Mimi ndiye Waziri wa Uchukuzi, nimekuja kujionea mwenyewe na kuchukue hatua. Ninawaahidi hali hii katika kipindi hiki cha uongozi wangu haitajirudia.
Nitahakikisha ndani ya muda mfupi kunakuwa na mabadiliko makubwa.”
Baada ya maelezo hayo, abiria hao walianza kuzungumza kwa mpangilio na kumweleza waziri huyo kuwa kitendo cha treini ya abiria kuchelewa kuondoka bila taarifa yoyote kinawasababisha usumbufu mkubwa.
Mmoja wa abiria hao, Paulo Michael alisema kama hali hiyo haitadhibitiwa inaweza kulipeleka taifa katika hali mbaya kwa kuwa wananchi wamechoka na kukataa tamaa.
“Mheshimiwa hivi sasa wananchi wamekata tamaa, kama watendaji wa mamlaka hii wataendelea kututesa namna hii …alilalamika Michael ambaye alionekana kukerwa na kitendo hicho.
Alisema watu wakiwamo wanawake na watoto, wanateseka kutokana na uzembe wa watu wachache na kwamba, jambo hilo ni hatari kwa usalama wa nchi.
Akijibu hilo, Dk Mwakyembe alisema; “Kuhusu hili nawahakikishia kuwa halitatokea tena katika kipindi changu, natambua mmeumia, lakini nawaahidi kufanya mabadiliko, nipeni muda mfupi.”
Abiria hao waliendelea kupaza sauti wakimtaka waziri huyo kutoondoka eneo hilo hadi watakapoondoka kwa kuwa watendaji hao wanaweza kuwadanganya.
Hata hivyo, Waziri Mwakyembe kabla ya ombi hilo la abiria alikuwa ameahidi kuwa hataondoka eneo hilo hadi treni litakapoondoka.
Dk Mwakyembe pia aliwahoji abiria hao kama kiwango cha nauli wanazolipa kinalingana na ubora wa huduma zinazotolewa.
Katika mazungumzo hayo alibaini kuwa kulikuwa na wanafunzi waliotozwa nauli ya watu wazima jambo alilokemea na kusisitiza kuwa asingependa kuona linaendelea.
Waziri huyo baada ya kuzungumza na abiria waliokuwa wanasafiri kwa daraja la tatu, alikutana na wa daraja la kwanza na la pili ambao wengi wao ni wageni kutoka nje ya nchi.
Baada ya kuingia katika ukumbi wa abiria wa daraja hizo kujitambulisha, wasafiri hao ambao baadhi walikuwa wamelala waliamka na kuhoji maswali juu ya sababu za kuchelewa na kama safari itakuwapo.
Dk Mwakyembe aliwajibu kuwa hali hiyo imetokana na uzembe wa watendaji na kuwahakikisha kuwa safari treni ipo na itaanza muda mfupi ujao.
Huku abiria hao wakimpongeza waziri huyo kwa ujasiri na uzalendo wa kuwatembelea usiku, baadhi yao walitoa kamera na simu zao kupiga picha za kumbukumbu.
Ahidi kutimua viongozi
Dk Mwakyembe aliahidi atawashughulikia watendaji wote wa mamlaka hiyo waliosababisha uzembe huo.
“Kama ingekuwa mamlaka yangu leo ningetangaza vinginevyo, lakini shirika hili linazihusu serikali mbili za Tanzania na Zambia. Hata hivyo, ili kusonga mbele mabadiliko ni lazima,” alisisitiza Dk Mwakyembe ambaye alifika hapo muda mfupi baada ya kurejea nchini, kutoka India.
Alisisitiza uzembe wa watendaji huo umefikia ukomo na aliahidi kufikisha mwenendo mzima wa utendaji wa mamlaka hiyo katika kikao cha Baraza la Mwaziri.
“Nimekuja kujionea mwenyewe hali hii na nimethibitisha kuwa tatizo ni uongozi. Suala hili nitalifikisha katika kikao cha Baraza la Mawaziri,” aliahidi Dk Mwakyembe. Awali Meneja Mkuu wa Tazara Kanda ya Tanzania, Abdallah Shekimweri alimweleza waziri huyo kuwa usafiri umechelewa kutokana na kuchelewa kupata mafuta ya dizeli.
“Tatizo ni mafuta, yamechelewa kupatikana kutokana na kumalizika mkataba baina yetu na kampuni iliyokuwa inatusambazia mafuta na mwenye uamuzi wa kusaini mkataba ni Mkurugenzi Mkuu ambaye hajafanya hivyo hadi sasa,” alisema Shekimweri.

CHADEMA YASUASUA....NA KUTIKISIKA!!!!!
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jana kiliteka jiji la Dar es Salaam kilipofanya mkutano mkubwa wa hadhara katika Viwanja vya Jangwani kwa lengo la kuzindua mkakati wake mpya unaojulikana kama ‘Movement For Change-M4C’ (Harakati za kuleta mabadiliko) ukiwa na lengo la kukiandaa chama hicho kuongoza dola mwaka 2015.
Katika mkutano huo uliohudhuriwa na maelfu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliwaonya watu aliowaita wasaliti ndani ya chama hicho, kwa kuwataka wajirudi mara moja, vinginevyo watashughulikiwa kwa mujibu wa taratibu.
Hivi karibuni Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda amekuwa akizozana na viongozi wa chama hicho tangu pale alipotangaza nia yake ya kuwania urais huku akimtaja Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kuwa atakuwa meneja wake wa kampeni. Bila kumtaja jina, Mbowe alianza kwa kutoa kauli zilionekana moja kwa moja kumjibu Shibuda, akisema wapo watu wanaodai kuwa Chadema ni chama cha udini na ukabila na kusisitiza kuwa huo ni uzushi.
Wakati akiendelea kusema hayo, umati uliokuwepo uwanjani hapo ulipokea kauli hiyo kwa kupaza sauti kwamba “Shibuda ang’olewe …Shibuda ang’olewe… Shibuda aondoke!’ hoja iliyojibiwa na Mbowe papo kwa hapo kwamba mkutano huo haukuwa na lengo la kumng’oa mtu.
“Sikuja hapa kumng’oa mtu…Tumng’oe?” Alihoji Mbowe na kuongeza: “Ngoja nitoe kauli ya chama. Chama chetu hakitayumbishwa na mtu yeyote msaliti. Tutatumia vikao vya chama. Tuzungumze mambo yenye maslahi ya taifa, siyo mtu mmoja mwepesi. Kama mtu hajui moto auchezee.” Alisisitiza kuwa chama hicho kimejengwa kwa zaidi ya miaka 20 na kimeweza kujenga ngome katika mikoa ya Mwanza Lindi na Mtwara. Huku akinukuu kauli ya Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela aliyoitoia miaka ya 1960, Mbowe alilitaka Jeshi la Polisi kutowatisha wanachama wa Chadema na kuonya kuwa wakifanya hivyo, wananchi nao watajibu mapigo. “Chadema kitakuwa chama cha mwisho kuvuruga amani nchini. Nawaonya kama Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na kama Mwenyekiti wa Chadema na kama Mbunge. Nawaomba polisi, waache kuwasumbua wana Chadema,” alionya Mbowe. Licha ya Jeshi la Polisi kuzuia maandamano ya wanachama wa chama hicho kikuu cha upinzani, watu walianza kufurika katika Viwanja vya Jangwani kuanzia saa 8:00 mchana. Kampeni ya Movement for Change(M4C) Akizungumzia mkakati huo, aliwataka wanachama wa Chadema na wananchi kwa ujumla kujitolea kukichangia fedha ili kufanikisha kampeni hiyo kwani alisema kukiondoa CCM madarakani si kazi rahisi, inahitaji gharama kubwa.
“Kila mwananchi anawajibu wa kubadilisha maisha yake. Kila mtu anapaswa kuwa wakala wa mabadiliko. Kuiondoa CCM kuna gharama kubwa, kule Arumeru watu walichanga kile walichokuwa nacho kuanzia Sh. 50 na kuendelea na tulishinda, au siyo? Tusije tukapata viongozi kwa fedha chafu,” alisema. Mbowe pia alisisitiza kuwa watakuwa makini na wanachama wa CCM wanaohamia Chadema akisema kuwa watatakaswa kwanza kabla ya kupewa uanachama. Kama hiyo haitoshi, chama hicho ‘kilitembeza bakuli’ kwenye mkutano huo, ambapo watu walichanga fedha kwa ajili ya kukisaidia katika utekelezaji wa mkakati huo ambao utafanyika nchi nzima. Awali, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, aliwapa somo wananchi kuhusu mchakato wa kuandikwa Katiba mpya. Alisema kuwa katiba ya sasa ni mbovu na kwamba inatakiwa ipatikane mpya ambayo haitachakachuliwa kwa ajili ya maslahi ya Watanzania huku akihoji mfumo wa utawala na suala zima la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. “Je, kuna nchi ngapi katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, kuna Amiri Jeshi wangapi katika Jamhuri hii? Hivi hii ni nchi moja au tunataka kuwa na katiba itakayojibu haya yote?” Alihoji Lissu. Aliwataka wananchi kuhoji Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba mpya kuhusu masuala hayo kwa kuwa Katiba mpya ya Zanzibar, inakinzana na Tanzania Bara na kwamba imefumua dhana nzima ya Muungano. “Watanzania wanatakiwa kupewa mamlaka ya kuamua kwa kupiga kura ya maoni ili kuona kama kuna haja ya kuwepo kwa Muungano au kuendelea na hiki kiini macho,” alisema Lissu. Alisema kuwa hata Bunge la Katiba ambalo litaundwa kwa ajili ya kujadili rasimu ya katiba itakayoandaliwa na Tume ya Katiba, linaweza kuchakachuliwa kwa kuwa na wabunge wengi wa CCM ambao watapitisha baadhi ya vipengele kwa maslahi ya chama hicho. “Kwa mtindo huu hatutapata Katiba mpya, yatakuwa yale yale, Sheria ya Marekebisho ya Katiba inatakiwa kufanyiwa marekebisho ili wabunge wa Bunge la Katiba wachaguliwe na wananchi” alisema Lissu. Alisema kuwa sheria hiyo inaeleza kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) ndio itakayosimamia kura za maoni na kwamba hali hiyo haitaleta Katiba mpya kwa kuwa Nec imegeuka kuwa Tume ya Taifa ya Uchakachuaji. Aliwataka wananchi kuhoji mamlaka aliyonayo rais kwa kuwa katiba ya sasa inampa mamlaka makubwa kiongozi huyo mkuu wa nchi ambaye anaweza kuamua lolote analotaka. “Inatakiwa kuwe na mfumo wa utawala utakaowapa nguvu wananchi,” alisema Lissu na kufafanua, “ Bunge limejaa zaidi ya wabunge 100 ambao hawajachaguliwa na wananchi, hivyo kazi yao ni kugonga meza tu, jengeni hoja zitakazoingizwa katika katiba mpya ikiwa ni pamoja na kulifanya Bunge kuwa na mamlaka ya kuiadabisha Serikali na ikiwezekana hata mkuu wa nchi”. Lissu alimataka Rais Kikwete kuheshimu ahadi aliyoitoa kwa viongozi wa Chadema waliokwenda Ikulu kupeleka maoni ya chama hicho kuhusu katiba. “Rais alitueleza wazi kuwa atafanyia marekebisho sheria ya mabadiliko ya Katiba kwa kuwa tuliilalamikia kwamba haikuwa sawa, ila naona hakuna alichokifanya, tunamuomba aheshimu ahadi yake,” alisema Lissu. Kwa upande wake Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willbroad Slaa ambaye tofauti na ilivyozoeleka, hakuzungumza kwa muda mrefu. Aliwataka wabunge wa chama hicho kuzungumzia matatizo yanayowakabili wananchi watakapokuwa bungeni mwezi ujao. “Maisha ya Watanzania si mazuri, vyakula vinauzwa kwa bei kubwa…, nitatumia nafasi hii kuwaeleza machache wabunge wangu ili wakayaseme bungeni, wabunge wetu hawana wa kuwafunga mdomo, maisha yanazidi kuwa magumu lakini yamekuwa mazuri kwa mafisadi, ”alisema Dk Slaa. Alisema kuwa Serikali inatakiwa itumie kodi ya wananchi kwa ajili ya shughuli za maendeleo na sio kuwalipa watumishi ambao nafasi zao hazina manufaa kwa wananchi. “Kuongeza kodi katika mafuta ya taa ili watu wasichakachue mafuta ya dizeli ni mwiba kwa Watanzania…, hii ni sawa na hoja ya mwendawazimu, wanatakiwa kudhibiti uchakachuaji sio kupandisha bei,” alisema. Dk Slaa pia aligusia mchakato wa Katiba mpya akiwataka wananchi kutoa maoni yao kuhusu mamlaka makubwa ya rais kwa kuwa ndio yanayochangia ugumu wa maisha kwa Watanzania. “Inakuwaje rais anateua mawaziri 55 halafu wananchi wanashindwa kuhoji, Uingereza mawaziri wapo 20 tu,” alisema Dk Slaa. Shamra shamra mkutanoni
Mbowe, Katibu wake Dk Slaa, wabunge na viongozi wengine walifika katika viwanja hivyo saa 9:30 na kufanya umati mkubwa uliokuwepo eneo hilo kulipuka kwa shangwe. Wabunge waliotia fora katika mkutano huo ni pamoja na Mbunge wa Ubungo John Mnyika tangu alipoingia uwanjani hapo na hata alipopewa nafasi ya kusalimia alishangiliwa kwa nguvu. Mnyika ambaye hivi karibuni alishinda kesi yake ya ubunge iliyofunguliwa na mpinzani wake kutoka CCM Hawa Ngh’umbi, alisema kesi hiyo imedhihirisha kuwepo kwa mfumo mbovu wa uchaguzi na kwamba madai yake kwamba CCM kimekumbatia mafisadi ni ya kweli. Aliyekuwa Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema naye alishangiliwa kwa nguvu hasa pale aliposema ni heri kuwa na vita vya kudai haki kuliko kuwa na amani inayopumbaza. Mkutano huo pia ulihudhuriwa na vyama marafiki kutoka nchi 16 za Afrika na baadhi ya viongozi kutoka chama tawala cha Ujerumani cha CDU. Chadema pia kiliendesha kampeni za ‘Vua gamba vaa gwanda’ ambapo kilivuna wanachama wapya 3,120 waliorudisha kadi zao wengi wakitoka CCM. Awali Chama cha CDU kiliendesha semina kwa viongozi wa Chadema kuhusu matumizi ya vifaa vya elektroniki katika masuala ya uchaguzi.

Wednesday, May 23, 2012
Sitta, Lowassa wazungumzia kujiunga na Chadema
SIKU chache baada ya aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema kuwataja mawaziri wawili na mmoja aliyewahi kuwa Waziri Mkuu kwamba, wameomba kujiunga na chama hicho cha upinzani, wawili kati yao wamejitokeza na kuzungumzia madai hayo.
Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ambao walitajwa na Lema, jana kwa nyakati tofauti walibeza madai hayo.
Jumamosi iliyopita, Lema akiwa wilayani Sengerema, Mwanza alisema mawaziri watatu, akiwamo mmoja aliyewahi kuwa waziri mkuu wameiomba kujiunga na Chadema lakini mmoja kati yao amekataliwa na wengine mchakato wa kuyakubali maombi yao unaendelea.
Katika mkutano huo, Lema aliwataja mawaziri hao kwa jina moja kuwa ni Sitta, Lowassa na waziri mwingine ambaye tunahifadhi jina lake kwa kuwa hakupatikana jana kuzungumzia madai hayo.
Msimamo wa Sitta
Sitta alipuuza madai hayo akiyaita ya kitoto na kueleza kuwa kwa hadhi yake, hawezi kuomba kujiunga Chadema na kusubiri majibu kama amekubaliwa au la.
“Yaani mimi niombe kwenda Chadema halafu nikae kabisa huku nikisubiri wanijibu! Huo ni upuuzi na jambo hili haliwezekani na si kweli hata kidogo. Kama Lema kasema hivyo, basi huo ni utoto na siasa za kihuni,” alisema Sitta.
Sitta huku akicheka aliongeza: “Sasa nimeomba kwa nani na kwa njia ipi ya mdomo au maandishi? Mimi siyo gamba. Ni mtu mwadilifu siwezi kujiunga katika utaratibu wa kuchukua magamba ndani ya CCM.”
“Wao Chadema wanachukua tu kila mtu. Wakienda kwenye mikutano pia wanachukua tu watu, sasa hivi wanachukua magamba CCM. Mimi nawatakia kila heri katika kuchukua magamba CCM.”
Sitta alisema yeye ni mwanasiasa makini na mwadilifu hawezi kukaa chungu kimoja na magamba... Wanalofanya kuchukua magamba ya CCM ni faraja hata kwa Katibu Mkuu Wilson Mukama.”
Mbunge huyo wa Urambo Mashariki, alisema kuchukua magamba CCM ni sawa na mtu ambaye anakwenda kwa jirani ambaye nyumba yake imezungukwa na takataka kisha akamsaidia kuzisomba kwenda kuzitupa... Hapo si lazima ufurahie bwana?
Alisema kama angekuwa anajiunga na Chadema wangemkumbatia akisema: “Kama wanakwenda watu wadogo wanaandaa sherehe kubwa, nikienda mimi...?
Majibu ya Lowassa
Jana, Lowassa naye alipuuza madai hayo ya Lema akisema hajawahi kuomba kujiunga na Chadema huku akisisitiza: “Kama ingekuwa hivyo isingekuwa siri. Ningetangaza uamuzi wangu kupitia vyombo vya habari.”
Lowassa alitoa kauli hiyo baada ya gazeti hili kumtaka azungumzie madai ya Lema kwamba aliomba kujiunga na chama hicho cha upinzani lakini akakataliwa.
“Kama ningeomba kuingia Chadema ningetangaza kwenye vyombo vya habari. Sijasikia hayo na sitaki kusema chochote zaidi,” alisema Lowassa na kisha kukata simu.
Slaa amshangaa Lema
Alipoulizwa kuhusu madai hayo ya Lema, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa alisema hawezi kuzungumzia kauli ya mtu.
“Tabia yangu huwa sipendi kuzungumzia kauli aliyoitoa mtu hivyo alichokisema Lema mtafuteni yeye mwenyewe afafanue kwani atakuwa anajua alichokisema kina maana gani,” alisema Dk Slaa.
Dk Slaa alisema: “Badala ya kukaa na kuzungumzia kauli ya mtu, kinachotakiwa ni kujadili jinsi gani ya kuhakikisha tunapunguza ugumu wa maisha kwa mwananchi wa hali ya chini.”
“Tuache kuzungumza kauli za watu hapa sasa kinachotakiwa kila mmoja wetu kwa nafasi yake atizame ni jinsi gani atahakikisha anamkomboa mwananchi kwa kupunguza gharama za maisha.”
Lema ang’ang’ana
Hata hivyo, jana alipotakiwa kufafanua kauli yake baada ya kuelezwa kwamba aliowataja wabeza madai yake, Lema aliendelea kusisitiza kwamba alichosema ni cha kweli.
“Wanakataa tu kisiasa, lakini nilichosema ni cha kweli na (kesho), leo katika mkutano wangu wa Singida, pamoja na kuwarudia hawa niliowataja nitawataja wengine pamoja na wabunge wa CCM ambao wapo tayari kujiunga na Chadema.”
Katika madai yake ya kwanza aliyotoa Jumamosi iliyopita katika mkutano uliofanyika kwenye Viwanja vya Mnadani, Lema alisema viongozi wenye uchungu na taifa hili ndani ya CCM na ambao wamekuwa hawafurahishwi na ubadhirifu wa mali za nchi, wamekuwa wakifanya mazungumzo kutaka kujiunga na Chadema.
Alisema kwa vile chama chake kimejiandaa kuingia madarakani kwa kutumia nguvu ya umma, ndiyo maana mawaziri wa Serikali ya CCM wameomba kujiunga nacho ili kusaidiana kwa pamoja kwenda kuingia madarakani mwaka 2015.
“Lakini, Lowassa tumemkataa. Tunataka wachapa kazi na wenye mioyo ya kweli katika mapambano ya kupigania haki na kuondoa dhuluma kwa Watanzania,” alisema Lema.
Lema alidai kuwa mawaziri hao (waliokubaliwa) wanasubiri muda muafaka ufike waweze kutangaza rasmi kujiunga na chama hicho, kutokana na kile kilichodaiwa kuchoshwa na mwenendo mzima wa uongozi na utendaji serikalini na ndani ya CCM, hususan suala la kuwalinda watu wanaotuhumiwa kwa ubadhilifu.
Frederick Katulanda, Mwanza; Fidelis Butahe na Ibrahim Yamola, Dar
UNAJUA KUWA MSANII JACQUELINE WOLPER AMILIKI MAGARI YA KIFAHARI..jembe hlo wana!!!!
Hili ni Toyota Noah lenye thamani ya Sh. milioni 18 ni kwa ajili ya kikazi zaidi
LISA JENSEN, OMMY DIMPOZ ‘IN LOVE’
Na Musa Mateja
KATIKA kuonesha kuwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya hasa masharobaro wamehamishia mapenzi yao kwa warembo, taarifa zilizotufikia zinadai Ommy Dimpoz yuko ‘in love’ na Miss Tanzania namba tatu 2006-07, Lisa Jensen.
Chanzo chetu cha kuaminika ambacho ni rafiki wa Ommy kimedai kuwa, wawili hao wana muda tangu wazame kwenye dimbwi la mahaba ila imekuwa ni kwa siri kubwa.
“Nyie si mnajua kufuatilia sana mambo ya watu? Sasa mbona mmeishia kuandika tu kwamba Diamond anatoka na Jokate halafu hamuandiki uhusiano wa Lisa na Ommy Dimpoz? Kama hamuamini fuatilieni mtaujua ukweli,” alisema mtoa habari huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Kujua ukweli wa ishu hii, mwandishi wetu alimtafuta Lisa ambaye alisema: “Duh! Kama demu wa Dimpoz ndiye anayenihusisha na madai hayo basi atakuwa na extra jealous (wivu wa kupitiliza), Dimpoz ni kaka tu.”
Kwa upande wa Dimpoz alifunguka: ”Lisa ni mshikaji wangu sana ndiyo maana napenda hata kuweka picha zake BBM, kama kuna lingine litajulikana tu.”
Souce:

Thursday, May 17, 2012
MHAADHIRI MATATANI KWA KUNASWA NA MTAMBO WA VYETI BANDIA!!
JESHI la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, linamhoji mhadhiri wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ushirika na Biashara Moshi (Muccobs), kwa tuhuma za kukutwa na vyeti vya kughushi vya vyuo vikuu kadhaa kwenye kompyuta yake.
Kukamatwa kwa mhadhiri huyo (jina tunalihifadhi), kumekuja siku chache baada ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), kuibua tuhuma nzito za kuwepo askari 948, kat
ika Jeshi la Polisi na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wenye vyeti bandia vya elimu.
Habari za uhakika kutoka Polisi na Muccobs, zinasema tayari kompyuta ya mhadhiri huyo ambayo ilikutwa na sampuli za vyeti hivyo, inashikiliwa na jeshi hilo kitengo cha makosa ya kughushi.
Taarifa hizo zimeeleza kuwa vyeti hivyo ni vya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (Saut) Mwanza, Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (Sua) Morogoro na ‘transcript’ za Muccobs.
Kukamatwa kwa mhadhiri huyo, kumekuja pia wakati kukiwepo kwa taarifa za kuzagaa kwa vyeti bandia vya Muccobs hususan ngazi ya stashahada ambavyo vinadaiwa kuuzwa kama njugu na mtandao mmoja ndani ya chuo hicho.
“Maneno yamekuwa mengi sana juu ya kuwapo kwa watu walioajiriwa katika taasisi mbalimbali nchini wakitumia vyeti vyetu, lakini hawajawahi kumaliza hapa kwetu,” alidokeza mhadhiri mmoja wa Muccobs.
Mkuu wa chuo hicho, Profesa Faustine Bee alithibitisha kukamatwa kwa mhadhiri huyo lakini akasema asingependa kulizungumzia jambo hilo kwa undani kwa kuwa linachunguzwa na polisi.
“Siwezi kusema kwa sababu hata hiyo kompyuta inayosemekana ilikutwa na vyeti hivyo, iko mikononi mwa polisi. Mkiwauliza polisi watakuwa na nafasi nzuri zaidi ya kulizungumzia,” alisema Profesa Bee.
Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro anayehamia Mara, Absalom Mwakyoma alipoulizwa jana alisema yuko safarini na kutaka aulizwe kaimu wake, Yusuph Ilembo lakini alipotafutwa alisema hafahamu jambo hilo.
Nahodha aahidi uchunguzi
Katika hatua nyingine, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha amesema atalifanyia kazi suala la vyeti vya kughushi lililowakumba askari wake.
Alisema hayo alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari baada ya kufungua mkutano wa Chama cha Kilimo Vijijini Afrika (Afraca), uliofanyika Dar es Salaam jana.
Nahodha alisema taarifa hizo za vyeti vya kughushi kwa askari wa JWTZ, amezisikia tu kwenye magazeti hivyo atazifuatilia.
“Nitasoma na nitafuatilia, nitalifanyia kazi na kujua ukweli na kama kutakuwa na ukweli wowote tutaushughulikia,” alisema Nahodha.
Wataka Mkuu wa Majeshi, IGP wajiuzulu
Chama cha siasa cha UPDP kimemtaka Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema na kuwajibika kutokana na sakata la baadhi ya watumishi wao kughushi vyeti.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa chama hicho, Fahmi Dovutwa alisema makamanda hao wameonyesha udhaifu mkubwa.
“Hii ni hatari kubwa hasa kwa usalama wa nchi yetu kama tunakuwa na wanajeshi ambao wameghushi vyeti halafu bado wanaendelea kuwepo kazini,” alisema Dovutwa.
Alisema suala la kutofanya ukaguzi kwa watu wanaowaongoza hadi kufikia baadhi yao kujinufaisha na vyeti bandia kwa miaka mingi ni udhaifu mkubwa kwa ulinzi nchini.
Mwenyekiti huyo alisema hali hiyo inatia shaka kwamba huenda kuna watumishi ambao si raia kwenye sekta nyeti nchini.
Askari hao walibainika kughushi vyeti hivyo wakati wa mchakato wa utengenezaji vitambulisho vya taifa na kusababisha kazi hiyo kushindwa kufanyika kama ilivyokuwa imepangwa.
Kwa mujibu wa Nida, vitambulisho hivyo vilitarajiwa kuanza kutolewa mwanzoni mwa mwezi huu lakini vimekwama kutokana na uhakiki uliokuwa ukifanywa katika fomu mbalimbali zilizokuwa zimejazwa.
Tayari Polisi na JWTZ wametangaza kuanza kufanya uchunguzi wa suala hilo ili kuwabaini wahusika na kuwachukulia hatua.
from www.mwananchigazeti.com

Ommy Dimpoz Kuzindua Single yake,’Baadae’ kiaina yake jumapili hii
Best Upcoming Artist wa Kilimanjaro Music Awards na mkali wa Nai Nai, Ommy Dimpoz, anatarajia kupiga show ya ukweli Jumapili hii kwa ajili ya kuzindua single yake mpya ya ‘Baadae’.
Akizungumza na son of maletho, meneja wa msanii huyo, Muba, amesema kwamba kwa sasa Ommy yuko busy anamalizia kupiga show za Kili Winners Tour ambapo ameshazuguka mikoa mingi ya Tanzania akikamua na washindi wenzake, na punde tu atakapomaliza mwishoni mwa wiki hii show yake ya Mbeya, atakamua Bilz kiania yake.
Ommy Dimpoz atasindikizwa na wasanii wenzake Ben Pol, mwandani wake Diamond Platnumz na wasanii wengine wengi.
Usimose super handsome jumapili ya tarehe 20 kule Bilz mtu wangu.

Utata wa umri wa Lulu watua Mahakama Kuu
MAWAKILI wanaomtetea mwigizaji wa filamu, Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu anayekabiliwa na kesi ya mauaji, wamewasilisha Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam maombi ya uchunguzi wa umri wa mteja wao.
Lulu anakabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake Steven Kanumba katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akidaiwa kutenda kosa hilo nyumbani kwa marehemu Machi 7, mwaka huu.
Mawakili hao waliwasilisha maombi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mei 7, mwaka huu wakiiomba iamuru kesi ya msanii huyo isikilizwe katika mahakama za watoto wakidai kuwa mteja wao ni mtoto.
Hata hivyo, mawakili hao waligonga mwamba baada ya mahakama hiyo kutupilia mbali ombi hilo ikisema ingawa kesi bado iko katika hatua za awali, haiwezi kufanya uchunguzi huo kwa kuwa haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo.
Jana, mawakili wanaomtetea msanii huyo waliwasilisha maombi Mahakama Kuu wakiiomba itoe uamuzi kama Mahakama ya Kisutu ina uwezo wa kuamua ufanyike uchunguzi wa umri halali wa msanii huyo kwa kuwa wanaamini kuwa ina mamlaka hayo.
Katika maombi hayo namba 46 ya mwaka 2012, yaliyosilishwa na Wakili Peter Kibatala kwa niaba ya jopo la mawakili hao, pia wanaiomba Mahakama Kuu kama itaridhika kuwa Mahakama ya Kisutu haina uwezo huo, basi yenyewe ifanye uchunguzi huo.
Akifafanua juu ya maombi hayo, Kibatala ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), alisema Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009, Kifungu cha 113 inaruhusu Mahakama kufanya uchunguzi wa umri wa mshtakiwa.
Wakili Kibatala alisema lengo la uchunguzi huo ni kuifanya ijiridhishe kama mshtakiwa ni mtoto au ni mtu mzima kwa lengo la kuangalia maslahi ya mtoto.
“Baada ya uchunguzi huo, mahakama ikijiridhisha kuwa ni mtoto, basi mwenendo wa kesi hiyo utaendeshwa kwa maslahi ya mtoto kwa mujibu wa Kifungu cha 4(2) cha Sheria ya Mtoto,” alisema.
Alisema kifungu hicho huelezea ulinzi na maslahi ya mtoto katika uendeshaji wa kesi kwa watoto wanaokinzana na sheria.
Mawakili hao wakiwa katika Mahakama ya Kisutu, walidai kwamba msanii huyo ana umri wa miaka 17 na kwa maana hiyo bado ni mtoto na kesi yake haipaswi kusikilizwa katika mahakama za kawaida kama mtu mzima.
Katika uamuzi wake, Hakimu Mkazi Augustina Mmbando anayesikiliza kesi hiyo alisema bado iko kwenye upelelezi na kwamba kulingana na jinsi ilivyo isingekuwa busara kuamua hoja yoyote na aliutaka upande wa utetezi uwasilishe maombi hayo kupitia Mahakama Kuu.
Wakati akiwasilisha maombi hayo awali Mahakama ya Kisutu, kiongozi wa jopo la mawakili wanaomtetea msanii huyo, Wakili Kennedy Fungamtama alidai kuwa mteja wao ana umri wa miaka 17 na si 18 kama inavyotamkwa mahakamani.
Alidai kuwa hata cheti cha kuzaliwa walichokiwasilisha mahakamani, kinaonyesha mahali na tarehe aliyozaliwa mshtakiwa hivyo kuwa na umri wa miaka 17.
Fungamtama alidai kuwa kulingana na Sheria ya Mtoto ya 2009, inatafsiri kuwa mtoto ni yule aliye na umri chini ya miaka 18 hivyo katika suala la mteja wao, alipaswa kushtakiwa katika mahakama ya watoto.
Hata hivyo, upande wa mashitaka kupitia kwa Wakili Elizabeth Kaganda ulipinga maombi hayo na kudai kuwa bado wanaendelea na upelelezi wa kesi hiyo na hivyo kuomba wapewe muda zaidi.
Wakili Kaganda pia alidai kuwa hata jina linaloonekana katika cheti cha kuzaliwa cha mshtakiwa huyo linasomeka kama Diana Elizabeth wakati mshtakiwa huyo ametajwa mahakamani hapo kama Elizabeth Michael.
Akijibu hoja hiyo, Wakili Fungamtama alikiri jina hilo kusomeka Diana Elizabeth na kusema kuwa ni jambo la kawaida hasa kwa Wakristo kuwa na majina mawili.
Mbali na Kibatala na Fungamtama, mawakili wengine katika jopo hilo ni Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG) Joaquine De- Melo.
Jopo la mawakili hao wanaomtetea msanii huyo linahitimishwa na Fulgence Massawe kutoka Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).
Kesi hiyo itatajwa tena mahakamani hapo Mei 21 mwaka huu na msanii huyo bado anaendelea kusota rumande kutokana na kesi inayomkabili kutokuwa na dhamana.

Wednesday, May 16, 2012
Mzee Makamba awarushia kombora Nape, Pinda
ASEMA NAPE ANAIGEUZA CCM MALI YAKE,PINDA YUKO MBALI NA WANANCHI, KINGUNGE PIA ACHARUKA!!!!
BAADA ya ukimya wa muda mrefu, Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Yusuf Makamba ameibuka katika kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho (Nec) na kumtuhumu Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye kwamba amekigeuza chama kuwa mali yake binafsi.
Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho, zimesema kwamba Makamba alisema hatua ya Nape kugeuza chama hicho kama taasisi yake binafsi ndiyo ambayo imesababisha kikose mwelekeo.
Makamba licha ya kuelekeza mashambulizi yake kwa Nape, alimrushia pia kombora Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuwa ana uhusiano mdogo na wananchi.
“Mzee (Makamba) amesema hivi sasa CCM imekuwa kama jogoo anayepelekwa kwa mganga, kila anakoelekezwa ndo huko, hali hiyo ndiyo inakikumba CCM hivi sasa. Amemweleza Nape kuwa amegeuza chama kama mali yake binafsi, anafanya mambo nje ya utaratibu na anaangaliwa tu.”
Makamba alidai kuwa badala ya sekretarieti kushughulikia matatizo ya chama, imekuwa ikihangaika na watu kwa sababu ya kutofautiana nao misimamo na wakati huo wakijidai kuzika tofauti ili kukiimarisha.
Nape alipoulizwa kuhusu suala hilo alipuuza na kusema: “Si kweli, lakini ninyi andikeni tu maana tumewazoea.”
Alipotakiwa kueleza kama Kingunge na Makamba walisema nini dhidi yake katika kikao cha Nec alijibu: “Walikuwapo, lakini hakuna kati yao aliyenitaja hata kwa jina.”
Nape alitumia muda mwingi kulalamika kuwa taarifa nyingi ambazo zimekuwa zikitolewa kutoka ndani ya mkutano huo uliomalizika jana zimetoka kwa watu aliowataja kuwa wana maslahi nazo binafsi na kuhoji,” Kwa nini msiwe mnasubiri taarifa rasmi (za chama) ili habari iwe ya ukweli zaidi?”
Mkongwe mwingine wa chama hicho, Kingunge Ngombale-Mwiru, ambaye anadaiwa kusikitishwa na vitendo vya rushwa na ugomvi vinavyoendelea ndani ya chama huku vikiangaliwa na viongozi kama vile vinakistawisha wakati vinakiporomosha.
Kingunge alidai kuwa hivi sasa chama hicho kimetawaliwa na matajiri ambao ndiyo wanaopata nafasi za uongozi na maskini wanawekwa kando.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja aliunga mkono suala la Pinda kuwa na uhusiano mdogo na wananchi na kwamba, amekuwa mkimya zaidi na hamsaidii Rais Jakaya Kikwete.
“Yule Mwenyekiti wa Shinyanga, amemweleza Pinda kuwa ng’ombe wakila mazao mtu wa kwanza kuchapwa viboko ni mchungaji, halafu mmiliki anatozwa faini baadaye. Hivyo, alitakiwa kuwajibika kwanza kabla ya mawaziri walioondolewa,” kilidokeza chanzo chetu.
Mgeja alidai kuwa uwajibishwaji wa mawaziri, haukuzingatia haki kwa sababu George Mkuchika, Profesa Jumanne Maghembe na Hawa Ghasia walilalamikiwa, lakini kilichofanywa ni kutoa kafara wengine na hao kubadilishiwa wizara.
Pia, inadaiwa kuwa Mwenyekiti Kikwete aliwataka wajumbe kuzika tofauti zao ili kuweka msimamo wa pamoja kwa ajili ya ushindi kwenye Uchaguzi Mkuu ujao wa 2015 na kwamba adui namba moja wa CCM hivi sasa ni Chadema.
Rushwa yakishtua chama
Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema Nec imejadili changamoto zinazokikabili chama kwenye uchaguzi unaoendelea na kubaini kuwa rushwa imekithiri.
Nape alisema tishio la rushwa ni kubwa na mgombea atayakayethibitika kujihusisha na vitendo hivyo rushwa ataondolewa mara moja, huku viongozi na watendaji wakitahadharishwa kuchukuliwa hatua za nidhamu.
“Kwa kisingizio cha kuwasalimia wajumbe, kuwapa nauli au kujitambulisha. Mgombea atakayethibitika anazunguka au amezunguka ataondolewa bila kuchelewa katika orodha ya wagombea,” alisema na kuongeza:
“Kwa watendaji na viongozi wa chama ngazi zote kuanzia sasa ni marufuku kuwatembeza ndani ya maeneo yao, kwa nia ya kuwatambulisha kwa wapiga kura. Mtendaji au kiongozi atakayebainika anakiuka agizo hili, atachukuliwa hatua za nidhamu mara moja.”
Pia, Nape alisema kuanzia sasa ni marufuku kwa watendaji na viongozi wa chama ngazi zote kuwaitia wagombea, wajumbe wa mikutano ya uchaguzi kwa lengo lolote, kwani vikao vya aina hiyo havimo katika katiba.
Alisema vikao vya aina hiyo ni haramu na vinapalilia rushwa na kuongeza kwamba wanachama wa CCM wanatakiwa kupiga vita rushwa na kutoa taarifa ya vitendo hivyo katika ofisi za chama na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
Aliitaka Takukuru kutomuonea aibu au kumuogopa mtu anayejihusisha na vitendo vya rushwa badala yake wamchukulie hatua.
Mishahara na chakula
Kuhusu mishahara ya watumishi wa umma na mfumuko wa bei ya chakula, Nape alisema Nec imeagiza Serikali kuhimiza waajiri kupandisha mishahara na malipo mengine kwa wafanyakazi wao ili waweze kumudu gharama za maisha.
Alisema gharama za maisha zimepanda na mishahara inayolipwa haiendani na hali halisi. Alisema nayo Serikali inatakiwa nayo kupandisha mishahara kwa watumishi wake.
“Serikali idhibiti malipo ya huduma ya ndani kwa kutumia fedha za kigeni, hasa Dola ya Marekani. Pia, iongeze udhibiti wa maduka na hoteli zinazofanya biashara ya fedha za kigeni ili kuondoa hujuma kwa uchumi wa nchi inayofanywa kutokana na uhuru uliokithiri katika biashara hii,” alisema.
Nape alisema Serikali inatakiwa kuweka jitihada zaidi za kudhibiti ulanguzi wa bidhaa muhimu na upandishaji holela wa bei za vyakula, kodi za nyumba na usafiri.
Alisema Nec imeagiza Serikali kuendelea kuchukua hatua za muda mrefu na kati za kukabiliana na tatizo la mfumuko wa bei.
“CCM inaiagiza Serikali kuchukua hatua za haraka na muda mfupi ikiwamo kuangalia upya baadhi ya kodi katika vyakula pamoja na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika sukari,” alisema Nape.
Pia, Nape alisema wameagiza Serikali kupitia upya utaratibu wa ruzuku ya mbegu na mbolea ili upanuliwe kunufaisha wakulima wengi.
Alisema Nec imeitaka Serikali iongeze kasi ya utekelezaji wa mpango wake wa kuongeza uwezo wa kuhifadhi chakula nchini, hasa kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Nafaka ya Taifa (NFRA), ikiwamo kujenga maghala zaidi ya mazao ya chakula maeneo ya uzalishaji na kutenga fedha nyingi zaidi kwa ununuzi wa mazao hayo.
“Wakati wa uhaba wa vyakula maeneo ya mijini, kasi ya kupeleka chakula maeneo hayo iongezwe na utaratibu mzuri zaidi wa usambazaji chakula utumike ili walaji na siyo wasafirishaji na wasindikaji, wanufaike,” alisema. from Midraji Ibrahim, Dodoma MWANANCHI GAZETI

Monday, May 14, 2012
HAPPPY MAMAS DAY...hongereni sana wakinamama...
mama ni mtu muhimu sana katika maisha yetu kama angeweza kuhesabu malezi na matunzo yote tangu utoto mpaka sasa u cant pay even for wat!!!i mic ma mum..na namshukuru sana kwakuwa alinifundisha maadili,kupenda na kujua dhamani ya mtu yeyote duniani...we real mic u mum ingawa haupo nasi tena but we still love u mum,,,said by all the family of maletho i,ken, jerry,nova,mage,lily,jack,her little twin my lovely baby gal adelyn{kajuku} and the big dady mzee maletho... REST IN PEACE MUM!!!!
Saturday, May 12, 2012
JAMAN!!!SAJUKI...mungu weka mkono wako..!!
AZIDIWA,ASHINDWA KUPOKEA MSAADA,VILIO CHUMBANI!!!
JAMAN SAJUKI! Siku mbili kabla ya kwenda katika Hospitali ya Apollo nchini India kwa matibabu, afya ya stadi wa filamu za Kibongo, Sadick Juma Kilowoko ‘Sajuki’ ni ya kusikitisha kupitiliza.Kadiri siku zinavyosonga, hali ya Sajuki inazidi kuwatoa watu machozi baada ya kuzidiwa na kushindwa kunyanyuka kitandani. Laiti kama utamuona na ukashindwa kububujikwa na machozi basi utakuwa huna utu.
ASHINDWA KUPOKEA MCHANGO
Tukio bichi kabisa lililowatoa machozi wasanii wenzake ni lile la Jumanne wiki hii nyumbani kwake Tabata Barakuda, Dar es Salaam ambapo msanii na prodyuza huyo wa filamu alishindwa kuamka kitandani kupokea dola elfu kumi (takribani Sh. milioni 15) alizozitoa mwigizaji mwenzake, Jacqueline Wolper kwa ajili ya matibabu huku akisindikizwa na mastaa wengine wa Bongo Movie.
The Udaku Master, Ijumaa lilimshuhudia Sajuki akiugulia maumivu huku akilalamika kujisikia vibaya, hivyo kuwaomba wasanii wenzake kwa heshima waingie chumbani kwake ili apokee fedha hizo.
WASANII VILIO
Kitendo hicho ndicho kilichowafanya baadhi ya wasanii wenzake kushindwa kujizuia na kujikuta wakiangua vilio huku Sajuki akiwatuliza na kuwaomba wasilie wala wasihuzunike kwani kila kitu ni mapenzi ya Mungu.
“Msihuzunike ndugu zangu, naamini kila kitu ni mapenzi ya Mungu na si vinginevyo, jipeni moyo,” alisema Sajuki kwa tabu akiwa amelala kitandani akiwa amezungukwa na mastaa hao.
WOLPER
Kwa upande wake Wolper aliyekuwa akimwaga machozi mithili ya bomba la mvua, alisema kuwa siyo kwamba ana fedha nyingi, ila ni namna alivyoguswa na mateso ya Sajuki.
“Siyo kwamba sina shida bali ni moyo wa kusaidia kuokoa uhai wa mwenzetu. Tulizoea kuwa naye location (sehemu ya kurekodia filamu) na kwenye tasnia yetu, anaumwa na hajiwezi, niliumia sana,” alisema Wolper aliyekuwa akifutwa machozi na wenzake.
WASTARA
Naye mke wa Sajuki, Wastara Juma, huku akilia muda wote, alitoa shukurani zake za dhati kwa Wolper na kueleza jinsi alivyoguswa na kuona umuhimu wa kumsaidia mumewe.
MASTAA
Baadhi ya mastaa wa Bongo Movie walioambatana na Wolper kuwasilisha mchango huo ni pamoja na Jacob Steven ‘JB’, Muhsein Awadhi ‘Dk. Cheni’, Chiki Mchoma ‘Chiki’, Hartmann Mbilinyi, Sabrina Rupia ‘Cathy’ na wengine.
HISTORIA UGONJWA WA SAJUKI
Taarifa za awali kabla ya Sajuki kuthibitisha ilielezwa kuwa alianza kwa kupata uvimbe sehemu tofauti katika mkono wake mmoja lakini baadaye tatizo hilo lilihamia ndani na kuanza kupata maumivu makali pembeni ya ini.
UNDANI WA UGONJWA
Kwa mujibu wa daktari aliyezungumza na Ijumaa (jina linahifadhiwa kwa sababu maalum), uvimbe pembeni ya ini ni dalili za ugonjwa alioutaja kitaalamu kama Hepatoma.
HEPATOMA NI NINI?
Daktari huyo alieleza kuwa Hepatoma ni moja ya kansa za ini ambayo huanzia kwenye sehemu ya juu kulia ya ini.
CHANZO
Ilifahamika kuwa chanzo cha Hepatoma ni magonjwa yanayoshambulia ini kwa pamoja, kitaalamu huitwa Hepatitis. Mbali na magonjwa hayo shambulizi, pia watu wanaotumia pombe, madawa ya kulevya wapo hatarini zaidi kupatwa na ugonjwa huo.
DALILI
Dalili za Hepatoma ni pamoja na maumivu makali sehemu ya juu ya kulia ya ini, kupoteza hamu ya kula, kukosa usingizi, kukondeana na kukosa furaha, yaani mtu wa ‘stresi’ muda mwingi.
MATIBABU
Mara nyingi njia ya upasuaji huwa chaguo la kwanza ili kuundoa uvimbe, dozi maalumu ya kutibu uvimbe huo na dawa za kutuliza maumivu.(from global publish mhariri:Imelda Mtema)
KILA LA HERI SAJUKI........katika safari ya india kwa matibabu!!!!
Man United yaikwanza rekodi yake England!!!!!!!
LONDON, England
WAKATI wachezaji wa Manchester City wakitoka nje ya uwanja na kipigo cha bao 1-0 toka Arsenal, Aprili 8, mashabiki wa timu hiyo hawakuamini kama mwezi mmoja mbele wangeweza kuwa kwenye nafasi nzuri ya kuweka historia jirani na kutwaa taji.
Kiwango kizuri walichoonyesha Arsenal kwenye mchezo huo, na kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa mshambuliaji Mario Balotelli, kuliwaacha mahasimu wa City, Manchester United wakiongoza kwa tofauti ya pointi nane na michezo sita ikisalia.
Ni wazi United walikuwa kwenye nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa, lakini sehemu ya kumalizia huenda ilikuwa tatizo kwa upande wao, na baada ya yote hayo walijikuta wakipata ushindi mmoja katika mechi nne zilizofuata.
Hiyo ilitoa mwanya kwa City kupanda kileleni mwa msimamo kwa tofauti ya mabao ya kufunga baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 mbele ya United Aprili 30 mwaka huu.
Hakuna timu iliyowahi kukosa ubingwa wakati ikiongoza kwa tofauti ya pointi nane kufikia Aprili.
Kocha Alex Ferguson amekutwa kile kilichomtokea farasi aliyejulikana kwa jina la Devon Loch aliyeangua mita 40 kabla ya kuvuka mstari wa mwisho wakati wa mashindano ya Mbio za Taifa za Farasi mwaka 1956.
Ferguson ana mashaka na matokeo hayo ambayo yamethibitisha udhaifu kwenye kikosi chake baada ya sare wasiyotarajia ya mabao 4-4 na Everton April 22 na kutoa mwanya kwa City kusogea zaidi kwa tofauti ya pointi tatu.
United wangeweza kuzoa pointi zote tatu kwenye mchezo dhidi ya Everton baada ya kuongoza 3-1 na kisha 4-2 kwenye Uwanja wa Old Trafford, lakini mwisho wa mchezo walijikuta wakiondoka na pointi moja.
"Nadhani mchezo dhidi ya Everton ulituua," alisema Ferguson. "Tulionyesha kiwango kibovu dakika 10 za mwisho. Kabisa, hatukuwa makini," alisema.
"Ni sahihi kusema historia ya United ni kushambulia muda wote wa mchezo, lakini tulicheza kizembe na hii imeturudisha nyuma, hakuna swali kwenye hilo. Ni mchezo dhidi ya Everton ndiyo uliotuharibia."
Kama City itaweka historia kwa kuwa timu ya kwanza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England kwa tofauti ya mabao ya kufunga, basi bila shaka maneno ya Ferguson yatawachoma zaidi wachezaji wake.
"Ni sawa kurejea kwenye vitabu vya historia ya United, lakini kuna wakati ukweli lazima uwe mbele," alisema Ferguson wakati fulani.
"Tulipokuwa tunaongoza 3-1, 4-1 tungetulia kwa idadi hiyo ya mabao. Lakini tuliendelea kushambulia badala ya kusema: 'Siku yetu imekwisha'."
Pamoja na yote hayo, hatua waliyofika United na City imeweka historia ya pekee katika soka la England ambayo inakaribiana na ile ya mwaka 1989 ambapo kulikuwa na ushindani mkubwa Ligi Daraja la Kwanza wakati huo kati ya Arsenal na Liverpool.
Msimu huu pia umekuwa na ushindani mkubwa, kwani mpaka sasa magoli 1,034 yamefungwa, huku zikisalia mechi 10, na kama kutakuwa na magoli 30 Jumapili wakati ligi ikifikia tamati, basi itazidi mabao ya msimu uliopita 1,063.

MADAWA YA KULEVYA...yanavyouzwa nje nje mjini dar..{KINONDONI}
KATIKA manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam yapo maeneo kadhaa ambayo mbali na kukaliwa na watu, yamebeba siri kubwa ambazo ni uihalifu wenye athari kubwa kwa maisha ya watu hasa vijana.
Kinondoni ni eneo maarufu ambalo si tu kwamba ni kubwa kwa wingi wa vitongoji vyake au wingi wa watu pekee, lakini hata kwa nyumba za starehe, maduka ya urembo na mavazi.
Kila unapotembea hatua kadhaa, utakutana na ama duka la nguo au baa. Lakini si hivyo tu, bali katika hatua hizo inawezekana ni tano, kumi, ishirini au zaidi ya hizo, aghalabu utakutana na mtu ambaye ana dalili za ulevi.
Wengi wa watu wanaoonekana kuwa wamelewa si kwa kunywa pombe, la hasha, bali ni ulivi wa dawa za kulevya. Huu ndio uhalifu ambao tunauzungumzia, kwani unaharibu sana maisha ya vijana kiasi cha kutisha.
Vyombo vya dola vipo na vinaona, viongozi wapo na wanaona, lakini hakuna kinachofanyika ni kama uhalifu huu umehalalishwa. Kutoka na hali hii gazeti hili lilisukumwa kufanya utafiti mdogo tu katika eneo la Kinondoni , kujua wapi kilipo chanzo cha umaarufu wa dawa hizi haramu.
Haikuwa kazi rahisi kwani kwa siku tatu mfululizo ilikuwa ni kazi ya kusoma mazingira ya baadhi ya maeneo yanayotajwa kutumika kuendesha biashara hiyo. Ilibidi zitumike mbinu mbalimbali kwani tuliambiwa kwamba ni hatari sana kufuatilia uhalifu huu.
Ni maeneo yapi?
Eneo la kwanza kugundulika lilikuwa ni lile lililoko maeneo ya karibu na hospitali ya Mwananyamala, nyumbani kwa maarufu, ambaye hata hivyo kwa sasa ni marehemu.
Watu wanavyoingia na kutoka ndani ya nyumba hiyo ni mithili ya nyuki wanavyoingia na kutoka kwenye mzinga wao. Hali hii inatupa ishara kwamba lazima kuna kinachofanyika ndani.
Nje ya nyumba hiyo, kuna miti kadhaa aina ya mwarobaini, magurudumu ya magari ambayo hutumiwa na wavutaji wa dawa za kulevya kujipumzisha nyakati zote na duka ndogo.
Ubavuni mwake zipo ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM) na mbele yake kuna soko dogo la wauzaji wa viazi mviringo na mikokoteni ya maji. Mpango wa kuingia ndani ya nyumba hiyo ulikamilika baada ya wiki moja, lakini tulipofanikiwa kuingia, tulibaini kuwa ina vyumba sita, vitatu kulia na vitatu kushoto.
Hata hivyo kuna baadhi ya vyumba vya uani ambavyo vinaonekana kuwa vimepangishwa. Ni vigumu kutambua nani anaishi chumba kipi kutokana na muingiliano, pia wingi wa watu.
Mara unapoingia unakaribishwa, maana wenyeji wanajua kwamba kila anayefika ni mteja wa bidhaa hiyo haramu. Hivyo baada ya kuketi, muuzaji anaitwa, anatoka ndani ya chumba cha pili kulia, kisha anauliza, “Unahitaji wa shilingi ngapi?”
Mwananchi linatoa noti ya Sh10,000 na yeye anahoji tena, “wa hela yote?.”
Muuzaji anatokomea na kurudi na karatasi lililosokotwa na kulikabidhi kwa mnunuzi.
Tunatoka nje ili kuondoka katika weneo hilo maana tumejawa na hofu kwamba huenda tukagundulika kwamba sisi siyo wateja, mara mmoja wa watu ambaye anaonekana kuwa mtumiaji aliyekubuhu wa dawa hizo anatutahadharisha kwamba tuwe makini kwani wakati mwingine tunaweza kuuziwa dawa ambazo si ‘kokaine au heroin.’
Tunapohoji ni dawa zipi ambazo zinaweza kuwa za kuchakachua, anatueleza kuwa, wakati mwingine wauzaji husaga mchanganyiko wa tembe za valium, fenegan, hamoxylin au piliton na kuziuza kama dawa za kulevya!.
“Wanachanganya na kusaga hizo dawa na wakikupa kama huujui unga halisi … utaingia mkenge, lakini unapata ‘stimu’ (unalewa) kama kawaida,” anasema.
Kazi nyingine
Katika nyumba hii si uuzaji wa dawa za kulevya pekee unaofanyika, bali pia zinafanyika shughuli za upakiaji na ufungaji wake tayari kwa kuuza.
Chanzo chetu cha habari kinaeleza kuwa, kila mara mzigo unapowasili, wapo vibarua ambao hutumiwa kufunga na kwamba wafungaji hawa mara nyingi ni watumiaji.
Anabainisha kuwa mfungaji hulipwa Sh200,000 kwa kufunga kete 50 na Sh400,000 kwa wanaoweza kufunga kete 100 za dawa hizo.
“Kufunga kwake ni kazi, ndiyo maana wanalipa bei ndefu (kubwa), kwa sababu, ule unga hauji kama unga, bali huja kama donge, kwa hiyo unatakiwa ulisage ili uuingize katika pakiti zake,” kilisema chanzo hicho.
Alisema, kuweka unga katika pakiti 50, huweza kumchukua zaidi ya saa sita. Chanzo hiki, bila kufahamu kinazungumza na nani, kilitoboa kuwa:
“Juzi nilitumwa nipeleke mzigo wa zaidi ya milioni sita kwa mzee anayeishi Mbezi, nilienda kwa pikipiki, nikalipwa laki moja na nusu,” alisema.
Akifafanua ni kwa namna gani yeye anaepuka kutumia dawa hizo, hasa wakati wa ufungashaji, alisema, huvaa gloves na kuufunika uso wake kwa kitambaa ili unga usiingie puani mwake.
Kikosi kazi Manyanya
Mwananchi lilibaini kuwa, kikosi kazi chenye mtandao mkubwa hufanya kazi katika kituo cha basi cha Manyanya kinachotumiwa na mabasi yanayoelekea Posta mpya.
Katika baadhi ya vibaraza vya maduka ya eneo hili, ndimo wanamoketi wauzaji. Ni vigumu kuwagundua wauzaji, lakini wanunuzi au watumiaji wanaonekana kwa macho kutokana na kulewa.
Kituo cha daladala cha Manyanya, kina idadi kubwa ya walioathirika na dawa hizi pengine kuliko kituo chochote hapa Dar es Salaam.
Utafiti wa Mwananchi ulibaini kuwa, baadhi ya maduka yaliyo pembezoni mwa kituo hiki ndimo zinapohifadhiwa dawa hizo. Ilibainika kuwa, dawa hizo huhifadhiwa katika maduka hayo, ili kurahisisha ununuzi kwa watumiaji.
Chanzo kingine kilibainisha kuwa: “Hapa wanafika watu wengi. Usifikiri wanakuja hawa wapiga debe tu. Hata wazee wenye heshima zao na magari yao, akina mama wenye familia, na watu wenye hadhi katika jamii,” anasema.
Wakati akieleza hayo, anatokea mwanamke wa makamo, anashuka katika gari. Chanzo chetu kinatupasha kuwa, huyo naye ni mtumiaji na aliwahi kuwa mke wa raia wa Uingereza.
Mwananchi liliendelea kuangaza na kuwaona baadhi ya vijana wakisaga dawa hizo kwa kutumia moto, vibati na kigae. Wengine wakiuvuta katika sigara na baadhi, wakinusa katika karatasi.
Aina mpya ya uvutaji
Mtoa habari mwingine aliliambia Mwananchi juu ya uvutaji mpya wa dawa za kulevya, ambao pengine waweza kuwa ni wa hatari zaidi kiafya.
Alisema, mtumiaji huchukua chupa tupu ya maji, kisha hujaza maji aidha nusu au robo ya chupa ile kisha hutumbukiza unga ndani ya maji yale.
Baada ya hapo, huchukua bomba la kalamu na kutoboa chupa, juu kidogo ya yalipoishia maji.Karatasi la foili au nailoni hufungwa katika mdomo wa chupa, bomba jingine la kalamu huchomekwa juu ya foili au nailoni.
“Ukimaliza unachoma moto bomba la kalamu, moto ukishika kasi na moshi ukianza kuingia ndani ya chupa, unavuta kwa kupitia bomba la chini,” alisema. Aliutaja mtindo huo kuwa unaitwa "wa kidosi/kitajiri' na wanaovuta dawa za kulevya kwa mtindo huo, hulewa kiasi cha kutojitambua na hujisaidia haja kubwa na ndogo.
“Siku hizi watu hawajichomi sindano, wanatumia njia hiyo, kunusa au kulamba,” alisema na kuongeza: "Huu mtindo unaleta raha ya ajabu, kiasi kwamba mtumiaji huweza kutumia hadi Sh 100,000 kwa siku moja tu."
Halikadhalika chanzo hicho kilikubali kutuuzia kete za dawa za kulevya kwa kutuahidi kutuletea hadi tulipoahidiana kukutana.
Wamiliki wa nyumba
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, mwenye nyumba hiyo alifariki miaka ya 80, aliacha wake wawili na watoto tisa, ingawa baadha wamekwishafariki.
“Mke mmoja wa yule mzee amefariki, lakini mwingine sijui habari zake,” kilisema chanzo hicho. Chanzo hicho kiliongeza kuwa, baada ya mzee huyo kufariki, nyumba hiyo ilibaki mikononi mwa watoto hao.
Miaka ya 90 hadi mwanzoni mwa miaka ya 2000, watoto hawa walijikita zaidi katika biashara ya pombe haramu ya gongo, baadaye bangi.Chanzo hicho kiliongeza kuwa, baadaye waliamua kuachana na uuzaji wa pombe na wakahamia katika uuzaji wa dawa za kulevya pamoja na bangi.
“Kaka yao mkubwa mwanzoni alikuwa analetewa kama msambazaji na kisha kuwauzia mateja, lakini baadaye akaanza kusafiri yeye mwenyewe,” kilisema chanzo hicho. Vyanzo hivyo vilidai kuwa, ndugu wote zaidi ya 10, wanafanya biashara hiyo, wakiwa na familia zao, na baadhi wakiwa ni watumiaji wakubwa.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Minazini, Juma Katogolo alikiri kuifahamu nyumba na familia hiyo ingawa alikana kufahamu biashara hiyo.
"Ninawafahamu, baadhi yao nimesoma nao, kwa mfano, huyo kijana mkubwa, (anamtaja jina) nimesoma naye darasa moja, lakini kujua biashara wanayofanya, siwezi kuthibitisha hilo," alisema Katogolo.
"Unajua hizi biashara hufanyika kwa usiri wa hali ya juu, siwezi kusema nina uhakika na hilo." Katogolo alisema amekuwa hapandezwi na tabia na vitendo vya vijana wa Wilaya ya Kinondoni kujitumbukiza katika utumiaji wa dawa hizo.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyella alisema hana taarifa na nyumba hiyo, isipokuwa polisi imekuwa ikifuatilia na kukamata dawa za kulevya kila siku.
“Ni ngumu kusema naifahamu nyumba hiyo lakini nisema tu kwamba Kinondoni kuwa sehemu ya jiji la Dar es
Salaam, tatizo la dawa za kulevya lipo kwa kuasi kikubwa,” alisema Kenyella.
Kamanda huyo aliendelea kueleza:”Polisi imekuwa ikifanya uchunguzi wake wa kiintelijensia na kwa kutumia msako wa kawaida na kufanikiwa kukamata aina mbalimbali za dawa kila siku.”Cocaine, “Tumekuwa tukikamata bangi, mirungi, heroine na cocaine kwa nyakati tofauti na kuzipeleka kesi hizo mahakamani.”
Hata hivyo Kamanda Kenyella alisema jitihada hizo zinarudishwa nyuma na baadhi ya watu ambao hawataki kushirikiana na polisi katika kuwafichua wahalifu hao.
“Wito wangu kwa jamii ni kwamba mjenga nchi ni mwananchi na mharibu nchi ni mwananchi mwenyewe. Naomba watu watusaidie kupata taarifa na sisi polisi tumekula viapo, tutazifanya taarifa hizo kuwa siri kabisa,” alisema{ kutoka kwa mwandishi wa mwananchi gazeti la tarehe 12/5/2012}

Subscribe to:
Posts (Atom)