Saturday, May 12, 2012

Msanii Dayna Chupchupu akumbwa na wimbi la Utapeli

Huku wimbi la utapeli likizidi kuwaandamana wasanii, mwanadada Dayna nae nusura kuingizwa mjini na mtu aliye jifanya ni msanii huyo kwa kutaka kujipatia pesa za shows zake.

Akiongea na maletho , Dayna amesema alijulishwa na watu wake wa karibu kwamba kuna mtu anatumia namba yake na kujifanya ni yeye. Alipochukua uamuzi wa kupiga namba yake, aligundua ni kweli na alipozungumza na dada huyo na kumdanganya anampa show, alijidai yupo Morogoro anamuuguza dada yake.

Dayna ameshawajulisha wahusika wake na vyombo vya dola kusudi mtu huyo achukuliwe hatua.

Dayna amethibitisha  na kutoa no ya huyo anayejiita Dayna feki mmumepuke, namba anayotumia tapeli huyo ni 0752872307

No comments:

Post a Comment