Thursday, May 31, 2012

Rais Kikwete ateua wakurugenzi wapya Mambo ya Nje....


 

RAIS Jakaya Kikwete ameteua wakurugenzi wapya tisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambao pia watakuwa na hadhi ya Balozi, akiwemo Msaidizi wa Rais (Hotuba), Mbelwa Kairuki. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mjini Dar es Salaam leo na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, uteuzi huo umeanza Mei 2, mwaka huu. Walioteuliwa ni Vincent Kibwana anayekuwa Mkurugenzi, Idara ya Afrika; Naimi Aziz (Idara ya Ushirikiano wa Kikanda); Celestine Mushy (Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa); Yahya Simba (Idara ya Mashariki ya Kati), na Bertha Somi (Idara ya Diaspora). Wengine ni Irene Kasyanju (Kitengo cha Sheria); Dorah Msechu (Idara ya Ulaya na Amerika); Kairuki ( Idara ya Asia na Australia), Silima Haji (Idara ya Mambo ya Nje, Zanzibar). Kabla ya uteuzi wake, Kibwana alikuwa Ofisa Mambo ya Nje Mkuu, Aziz alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Mushy alikuwa Kaimu Katibu wa Waziri Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Simba alikuwa Ofisa Mambo ya Nje Mkuu, na Somi alikuwa Ofisa Mambo ya Nje Mkuu. Naye Kasyanju alikuwa Mkurugenzi Msaidizi; Msechu alikuwa Mkurugenzi Msaidizi na Kairuki alikuwa Msaidizi wa Rais (Hotuba), Ofisi ya Rais, Ikulu na Haji alikuwa Ofisa Mambo ya Nje Mkuu.

No comments:

Post a Comment