MWANAMUZIKI nyota Tanzania, Diamond amesema kwamba kufanya kwake vizuri katika mahojiano aliyofanyiwa Kiingereza kwenye jumba la Big Brother Jumapili nchini Afrika Kusini, kulitokana na mafunzo mazuri ya kuzungumza lugha hiyo, aliyopewa na mpenzi wake wa zamani, Wema Sepetu.
Diamond ameyasema hayo leo mchana katika kipindi cha XXL cha Clouds Radio- baada ya kuulizwa siri ya kujiamini kwake kuzungumza vema Kiingereza bila kitete alipokuwa akihojiwa BBA.
"Namshukuru sana mama yangu mzazi aliyenisomesha, lakini pia namshukuru Wema Sepetu English Course, kwa kweli alinisaidia sana wakati nipo naye kunifundisha kuzungumza Kiingereza kwa kujiamini,"alisema Diamond.
Diamond anakuwa msanii wa pili kuzungumza hadharani kunufaika na lugha ya Kiingereza kutoka kwa Wema, baada ya marehemu Steven Kanumba naye kuwahi kusema hapo awali, alisaidiwa mno na Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006 kunyoosha lugha huyo
No comments:
Post a Comment